Barbara Serra
Barbara Serra (alizaliwa Milano, 1975) ni mzaliwa wa Italia anayeishi Uingereza mwandishi na mtangazaji habari, anayetangaza kutoka ofisi ya Al Jazeera iliyo mjini London.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Ingawa alizaliwa Milan kutoka kwa wazazi wa Kiitaliano, alikulia mjini Copenhagen kuanzia umri wa miaka tisa. Kwa ajili hiyo, Serra ana ujuzi wa lugha tofauti tofauti, lugha yake mama ikiwa Kiitalia, na nyinginezo kama Kiingereza, Kideni, na Kifaransa.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1993, alihamia Uingereza kusoma Uhusiano wa Kimataifa katika London School of Economics, na kisha akapata masomo ya kitaalam ya uandishi wa habari kupitia Diploma ya Uandishi Habari kutoka Chuo Kikuu cha City, mjini London. [1]
Serra alianza kazi ya uandishi habari na BBC, na mwishowe akawa mtafiti. Aliwahi kuwa mtayarishaji na mwanahabari wa BBC London News kwa muda wa miaka mitatu, alitayarisha kipindi cha Today Programme kwenye Radio 4 na mara kwa mara akatangaza habari kwa EuroNews kwenye BBC Radio Five Live. Changamoto aliyopata wakati wa kutangaza habari ni pindi alipotangaza habari kwenye redio na akalazimishwa kuongeza dakika tanoza utangazaji kwa ajili ya shida ya kiteknolojia.
Mwaka 2003, alijiunga Sky News kama mwandishi habari, akiripotia kuhusu habari za nchini na za duniani. Serra aliripotia hadithi tofauti, kama kifo cha Pope John Paul II huko Roma, na majaribio ya Michael Jackson katika jiji la California.
Mnamo Julai 2005, kama sehemu ya mpango wa Sky News alikuwa mtangazaji wa Five News.
Serra aliacha kazi Five News mnamo Aprili 2006, ilipotangazwa kwamba amejiunga na Al Jazeera ya Kiingereza kama mmoja wa wanahabari kutoka mjini London.[2] Yeye hutangaza matukio kutoka kote Ulaya, na vipindi kama People & Power na Streetfood Palermo.
Mnamo Septemba 2007, alianza kutangaza kwenye stesheni ya RAI, iliyopo Italiano, kwenye kipindi cha TV Talk kutoka kwa ofisi ya Al Jazeera ya London.
Maisha ya Kibinafsi.
[hariri | hariri chanzo]Serra ameolewa na mwanasheria aliyekuwa mwandishi wa Sunday Times Marko Austin mwezi Julai 2008. Wanandoa wanaishi jijini London.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [1] ^ Barbara Serra joins Al Jazeera International Ilihifadhiwa 13 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
- ↑ [2] ^ Al Jazeera International announces Barbara Serra | Appointments Ilihifadhiwa 9 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.