Baraza la mawaziri Tanganyika 1961
Mandhari
Baraza la mawaziri Tanganyika 1961 lilikuwa la kwanza baada ya Tanganyika kupata uhuru kamili kutoka hali ya nchi lindwa chini ya Waingereza iliyokuwa nayo hadi tarehe 9 Desemba 1961.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kupata uhuru mwaka 1961, Tanganyika ilikuwa na Baraza la mawaziri lenye mawaziri 11 tu, idadi ndogo kuliko serikali zote zilizofuata.
Mawaziri ni wafuatao:
- Waziri mkuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
- Waziri asiye na wizara maalumu Rashidi Mfaume Kawawa,
- Waziri wa elimu Oscar Kambona,
- Waziri wa serikali za mitaa Job Lusinde,
- Waziri wa mawasiliano, nguvu za umeme na ujenzi Amir Jamal,
- Waziri wa biashara na viwanda Nsilo Swai,
- Waziri wa ardhi na upimaji Tewa Saidi Tewa,
- Waziri wa sheria Chief Abdalah Said Fundikira,
- Waziri wa afya na kazi Dereck N. M. Bryceson,
- Waziri wa kilimo Paul Bomani,
- Waziri wa fedha Ernest Vassey na
- Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Clement G. Kahama.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Baraza la mawaziri Tanganyika 1961 kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |