Barakoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Barakoa ya Kiafrika.

Barakoa (pia: barkoa) ni kitambaa au kinyago kinachovaliwa usoni au kichwani chenye tundu kwenye macho, pua na mdomo linalotumiwa kukinga uso.

Mfano mmoja wa barakoa ni Barakoa ya Sirige ya Wadogon wa Mali.

Ni pia nguo ya wanawake wa Kiislamu ambayo wanaivaa kwenye mapaji ya nyuso zao pamoja na buibui, ijulikanayo kama "burqa".

Kuna barakoa za kinga zinazovaliwa kwa shughuli mbalimbali, zinazolenga kuzuia au kupunguza athira hatari za vumbi, gesi, hewa chafu au viini vya ugonjwa.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barakoa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.