Baikonur
Mandhari
Baikonur (kwa Kikazakhi: Baıqonyr / Байқоныр; kwa Kirusi: Байконур) ni jina la miji miwili nchini Kazakhstan.
- Baikonur ya kiasili ni mji mdogo kando ya mto Baikonur katika mkoa wa Karaganda uliokuwa na wakazi 427 kwenye mwaka 2009; kuna migodi ya makaa mawe.
- Baikonur unaojulikana kimataifa kama kituo cha kurushia vyombo vya anga-nje ni mji kwenye ukingo wa kaskazini wa mto Syr Darya. Umekodishwa na kutawaliwa na Shirikisho la Urusi.
Kituo cha kurushia roketi kilianzishwa mnamo mwaka 1955 karibu na kijiji cha Tyutaram wakati Kazakhstan ilipokuwa jamhuri ndani ya Umoja wa Kisovyeti; mwanzoni Umoja wa Kisovyeti ulijaribu kuficha mahali pake na baada ya mafanikio ya kwanza jina la "Baikonur" lilitangazwa hadharani kama mahali pa kurushia roketi. Mji ulikua hapa kwa makazi ya wanasayansi na wafanyakazi wa kituo. Ndani ya Umoja wa Kisovyeti walitumia pia jina la Звездоград (Zvezdograd) yaani "mji wa nyota"[1].
Tangu mwaka 1995, Urusi ilitumia rasmi jina la "Baikonur" kwa ajili ya mji huo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Barensky, C.; Lardier, Stefan (2013). The Soyuz launch vehicle the two lives of an engineering triumph. New York: Springer. uk. 189. ISBN 978-1461454595.