Azimio la kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake
Mandhari
Azimio la kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake (kwa kifupi DEDAW[1]) ni azimio la haki za binadamu lililotolewa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, linaloelezea maoni juu ya haki za wanawake. Lilipitishwa na mkutano mkuu mnamo 7 Novemba 1967.[2] Azimio hilo lilikuwa kichocheo muhimu cha mkataba wa 1979 wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW).
Lengo lake lilikuwa kukuza usawa wa kijinsia, hasa kwa ajili ya ulinzi wa haki za wanawake. Liliandaliwa na Tume ya Hali za Wanawake mwaka wa 1967.[3] Ili kutekeleza kanuni za azimio hilo, CEDAW ilianzishwa na kutekelezwa Desemba 3, 1981.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Freeman, Marsha A.; na wenz. (2012). The UN Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women: A Commentary. Oxford: Oxford University Press. uk. 38. ISBN 9780199565061. Iliwekwa mnamo 14 Machi 2020.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ United Nations General Assembly Resolution 2263, 7 November 1967.
- ↑ Evatt, Elizabeth (2002). "Finding a voice for women's rights: The early days of CEDAW". George Washington International Law Review. 34: 515–553 – kutoka Proquest Central.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |