Ayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ayo

Ayo (kwa jina la kuzaliwa Joy Olasunmibo Ogunmakin) ni mwimbaji nchini Ujerumani. Amezaliwa 14 Septemba 1980 katika kitongoji cha mji wa Cologne, Ujerumani. Ana asili wa mchanganyiko: yeye ni binti wa baba Mnigeria na mama anayetoka Romania.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Anatumbuiza kwa kutumia jina la kisanii la Ayọ au Ayo. Maana yake ni "furaha" kwa Kiyoruba. (Bila nukta chini au baada ya "o" neno lamaanisha "kitungu" katika lugha hiyo.)

Aliwahi kuishi Ujerumani, Nigeria, Ufaransa, Uingereza na Marekani. Anaishi pamoja na mwimbaji Mjerumani wa muziki ya Reggae Patrice Bart-Williams ("Babatunde") na mtoto wao wa pamoja Nile (*2005)

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Albamu yake ya kwanza, 'Joyful', imetolewa mwaka wa 2006. Katika Poland na hata Ufaransa imekuwa ikiuzwa nakala lukuki.

Vibao vyake vilivyo maarufu ni pamoja na 'Down on my knees' ('Nikikupigia Magoti', 2006) na 'And It's Supposed To Be Love' ('Na Hayo Yaelekea Kuwa Mapenzi', 2007).

Albamu 'Gravity At Last' (2008)

Albamu 'Billie-Eve' (2011)

Albamu 'Ticket to The World' (2013)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: