Asa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Asa alivyochorwa na Guillaume Rouillé mwaka 1553.
Asa akibomoa sanamu.

Mfalme Asa (kwa Kiebrania: אָסָא, ʾAsaʾ au ʾĀsāʾ; 930 KK hivi - 870 KK hivi) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 911 KK na 870 KK.

Muda huo alijitahidi kurudisha Israeli kwa Mungu pekee, YHWH, kama alivyoelekezwa na Nabii Azaria.

Kwa ajili hiyo, nchi ilifurahia amani miaka 35.

Mwishowe alimdhulumu nabii Hanani na kuwategemea matabibu kuliko Mungu katika ugonjwa wa miguu yake.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 14-16.

Pia anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

      . https://books.google.com/books?id=S4MZREX03u0C&pg=PT30.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asa kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.