Arkadi, Paskasi na wenzao
Arkadi, Paskasi na wenzao Probo, Eutikiani na Paulilo (karibu wote walifariki Afrika Kaskazini, 437) ni kati ya waumini wa Kanisa Katoliki walioteswa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Genseriki aliyekuwa Mwario.
Wazaliwa wa Hispania, walikuwa askari wa mfalme huyo, Paskasi na Eutikiani walikuwa ndugu na Paulilo alikuwa mdogo wao.
Walipokataa katakata kujiunga na Uario, walifilisishwa, walipelekwa uhamishoni, waliteswa kikatili na hatimaye kuuawa kwa namna mbalimbali, isipokuwa mtoto Paulilo. Hata yeye alionyesha msimamo imara katika mani sahihi kwa sababu alipigwa fimbo muda mrefu na hatimaye alifanywa mtumwa[1].
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 13 Novemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |