Apolinari wa Ierapoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Apolinari wa Ierapoli (pia: Apolinari Klaudio au Apolinari Mtetezi wa Dini; alifariki karne ya 2) alikuwa askofu aliyeongoza kanisa la Ierapoli na kumuandikia kaisari Marcus Aurelius "Apologia", kitabu cha kutetea Wakristo dhidi ya dhuluma ya Dola la Roma (177)[1].

Aliandika pia vitabu vingine dhidi ya Upagani na uzushi. Hata hivyo zimetufikia sehemu chache, ile ndefu zaidi ikihusu tarehe ya Pasaka.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Januari[2][3].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.