Antonio Valencia
Youth career | |||
---|---|---|---|
1999–2001 | Caribe Junior | ||
2001–2004 | El Nacional | ||
Senior career* | |||
Miaka | Timu | Apps† | (Gls)† |
2003–2005 | El Nacional | 84 | (20) |
2005–2008 | Villarreal | 2 | (0) |
2005–2006 | → Recreativo (loan) | 14 | (1) |
2006–2008 | → Wigan Athletic (loan) | 37 | (1) |
2008–2009 | Wigan Athletic | 47 | (6) |
2009– | Manchester United | 17 | (4) |
Timu ya Taifa ya Kandanda‡ | |||
2005– | Ecuador | 40 | (6) |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 15:06, 20 Desemba 2009 (UTC). † Appearances (Goals). |
Luis Antonio Valencia Mosquera (anayejulikana sana kama Antonio Valencia; alizaliwa 4 Agosti, 1985) alikuwa mchezaji wa kandanda, kiungo cha kati mwenye uraia wa Ecuador ambaye alichezea klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ecuador.
Wasifu wa Klabu
[hariri | hariri chanzo]Wasifu wa Mapema
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuwa na utoto ambao haukujaliwa katika sehemu ya Lago Agrio, Valencia alianza wasifu wake katika klabu ya El Nacional na alihamia timu ya ligi ya Kihispania, Villarreal, mwaka wa 2005. Hata hivyo, alipeanwa kama mkopo katika klabu ya Recreativo de Huelva muda mwingi wa msimu wa 2005-06, ambapo aliisaidia timu kupanda cheo kucheza katika ligi kuu ya Uhispania.
Wigan Athletic
[hariri | hariri chanzo]Mwanzoni mwa msimu uliyofuata, alijiunga na klabu ya Ligi ya Uingereza, Wigan Athletic, awali kama mpango wa mkopo kwa muda wa mwaka moja. Alicheza mechi yake ya kwanza ya Wigan tarehe 19 Agosti 2006, mechi ambayo Wigan ilipoteza 2-1 dhidi ya Newcastle United, na aliifungia Wigan bao lake la kwanza dhidi ya Manchester City tarehe 21 Oktoba 2006. Muda wa mkopo uliongezwa hadi msimu uliyofuata, na tarehe 18 Januari 2008 alihamia Wigan rasmi kwa kitita cha ada ambacho hakikutangazwa, na alisaini mkataba wa miaka tatu unusu. Alikataa kuihamia timu ya La Liga ya Real Madrid mnamo Januari 2009. Mapema juni mwaka wa 2009, mwenyekiti wa Wigan alitangaza kuwa hatamlazimisha Valencia kubaki katika klabu.
Manchester United
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 30 juni 2009, Valencia akawa mchezaji wa kwanza kusainiwa na klabu ya Manchester United, na alikatiza likizo yake kwa ajili matibabu na klabu. Alisaini mkataba wa miaka minne kwa kitita cha ada ambacho hakikutangazwa, lakini fununu ni kuwa ada hiyo ilikuwa ya paundi milioni (£) 16. Alicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani ya Manchester United katika FA Community Shield mwaka wa 2009, wakati aliingia kama mbadala wa Nani katika dakika ya 62 wakati Nani alijeruhiwa. Tarehe 17 Oktoba 2009, alifunga bao lake la kwanza la klabu, kwa kufunga bao la upili na la ushindi katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bolton Wanderers [25] Bao lake la kwanza katika shindano la kombe la mabingwa barani Ulaya lilifuata siku nne baadaye katika ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya CSKA Moscow. Tarehe 15 Desemba, Valencia alifunga bao katika mechi yake ya 100 ya Ligi Kuu ya Uingereza na bao lake liilikuwa la mwisho katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Wolves.
Wasifu wa Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Valencia aliichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza katika mechi ya kufuzu kushiriki katika Kombe la Dunia la FIFA dhidi ya Paragwei tarehe 27 Machi 2005, na alifunga mabao mawili katika ushindi wa 5-2. Aliichezea Ecuador katika kombe la dunia la 2006, na alichaguliwa kama mteule wa timu ya FIFA ya wachezaji 11 bora, ambayo inatambua wachezaji nyota katika kila nafasi katika Kombe la Dunia. Pia aliorodheshwa kama mmoja wa wagombea sita kwa tuzo la mchezaji bora mchanga wa Gillette. Barua pepe lilisambazwa nchini Uingereza na liliwapa moyo watu kumpigia kura Valencia, katika jaribio la kuzuia Cristiano Ronaldo kushinda. Valencia alipokea idadi kubwa ya kura katika uchaguzi wa mtandao wa tarakilishi, [34] lakini tangu Mshindi wa tuzo anadhamiriwa na kura za wafuasi na jopo la majaji, hatimaye tuzo alipewa Lukas Podolski.
Takwimu ya Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Takwimu ya wasifu nchini Uingereza
Klabu | Msimu | Ligi! | Kombe! | Kikombe cha Carling | Continental | Nyingine [1] | Jumla | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | ||
Wigan Athletic | 2006-07 | 22 | 1 | 0 | 0 | 0 | 0 | -- | 0 | 0 | 22 | 1 | |
2007-08 | 31 | 3 | 1 | 0 | 0 | 0 | -- | 0 | 0 | 32 | 3 | ||
2008-09 | 31 | 3 | 1 | 0 | 3 | 0 | -- | 0 | 0 | 35 | 3 | ||
Jumla | 84 | 7 | 2 | 0 | 3 | 0 | -- | 0 | 0 | 89 | 7 | ||
Manchester United | 2009-10 | 17 | 4 | 0 | 0 | 1 | 0 | 5 | 2 | 1 | 0 | 24 | 6. |
Jumla | 17 | 4 | 0 | 0 | 1 | 0 | 5 | 2 | 1 | 0 | 24 | 6. | |
Jumla wa wasifu | 101 | 11 | 2 | 0 | 4 | 0 | 5 | 2 | 1 | 0 | 113 | 13 |
Takwimu sahihi kama ya kucheza mechi 19 Desemba 2009. [2]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Klabu
[hariri | hariri chanzo]- El Nacional
- Serie A de Ecuador (1): 2005 Clausura
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [18] ^ Yajumuisha ushindani wa mashindano mengine, zikiwemo FA Community Shield, Uefa Super Cup, kombo la intercontinental , FIFA Club World Cup
- ↑ Endlar, Andrew. "Antonio Valencia". StretfordEnd.co.uk. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2009.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Luis Antonio Valencia career stats kwenye Soccerbase
- Luis Valencia FIFA competition record
- Antonio Valencia profile at the Manchester United website