Antonio José de Sucre
Mandhari
Antonio José de Sucre (3 Februari 1795 - 4 Juni 1830) alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa wa Amerika Kusini akipigania uhuru wa nchi mbalimbali pamoja na rafiki yake wa karibu Simon Bolivar. Alikuwa Rais wa sita wa Peru kuanzia tarehe 23 Juni hadi 17 Julai, mwaka wa 1823. Tena alimfuata Simon Bolivar kuwa Rais wa pili wa Bolivia kuanzia tarehe 29 Desemba 1825 hadi 18 Aprili 1828. Alijiuzulu na kuhamia mjini Quito. Aliuawa kwa kupigwa risasi aliposafiri karibu na mji wa Pasto nchini Colombia.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Antonio José de Sucre kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |