Angela Okorie
Angela Okorie | |
---|---|
Angela Okorie | |
Amezaliwa | Angela Ijeoma Okorie Oktoba 29 1975 Cotonou, Benin |
Kazi yake | Muigizaji |
Miaka ya kazi | 2009 mpka sasa |
Ndoa | Ameolewa |
Watoto | mmoja |
Angela Okorie ni mwigizaji wa Nigeria.[1] Mwaka 2015 alishinda City People Entertainment Awards katika nafasi ya Mwigizaji Bora anayeunga Mkono. Pia anatambulika katika kuigiza zaidi ya filamu 100 kati ya mwaka 2009 na 2014.
Maisha ya awali na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Okorie, mtoto wa tatu kati ya watano, ni mtu asili wa Ishiagu ndani ya Ivo LGA ilioko Ebonyi State.[2] lakini alizaliwa na kukulia Cotonou, Benin. Alisomea sanaa ya ukumbi wa michezo katika Chuo Kikuu cha Lagos.[3] Pia alihudhuria Lagos State University, alipokuwa akisomea public administration.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Okorie alijiunga na Nollywood mwaka 2009, baada ya miaka kumi ya kutengeneza modeli katika kampuni ya sabuni. Filamu yake ya kwanza ilikuwa Sincerity mwaka 2009.[2] Filamu ilitayarishwa na kuelekezwa na Stanley Egbonini pamoja na Ifeanyi Ogbonna, na mhusika mkuu Chigozie Atuanya, Nonso Diobi, Yemi Blaq na Oge Okoye. Kulingana na Pulse Nigeria, mwangaza wake ulionekana alipokuwa mhusika mkuu katika Holy Serpent. Pia alisema kuwa ana pendekezo la kurekodi miziki ya injili hapo baadaye.[3] Mwaka 2014, alitambuliwa kama miongoni mwa “waigizaji wanaotafutwa zaidi” katika Nollywood kutokea katika gazeti la Vanguard, vile vile kama “mwigizaji maarufu” anaetekeleza majukumu kwa urahisi kupitia gazeti la The Nation.[2] Pia alisema kuwa anatarajia kuingia katika utayarishaji wa filamu. Kuzungumzia matarajio yake ya muziki, alieleza kuwa aliandika nyimbo kadhaa na angeachilia albamu yake karibuni, akitambulisha muziki kama kitu kilichokuwa miongoni mwa matarajio yake.[4] Ilipofika Januari 2014, aliwekwa katika kumbukumbu kwa kuigiza zaidi ya tayarisho za filamu 80.[2] Mwaka 2015, alishinda City People Entertainment Awards katika nafasi ya Mwigizaji Bora anayeunga Mkono katika filamu za Kiingereza.[5] Ndani ya Agosti 2014, aliigiza zaidi ya filamu 100 toka 2009. Katika mahojiano ya 2014, alieleza kuwa mama yake hakujisikia vizuri na uigizaji wake katika misingi ya kidini. Alisema kuwa asingeweza kuigiza uchi bila kujali malipo, akieleza kuwa hata wale aliowaiga katika tasnia ya Nigeria, kama Genevieve Nnaji hawakuhitaji kufanya hivyo kuwa maarufu. Alitaja pia imani zake za kitamaduni kama sababu za kuvaa kihafidhina katika filamu.
Maisha binafsi na maoni juu ya usagaji
[hariri | hariri chanzo]Ameolewa na ana mtoto. Katika chapisho la gazeti la Daily Post (Nigeria), ameeleza kuwa anatumia juhudi sana kutenganisha familia yake na vyombo vya habari. Pia alikanusha habari za uvumi za mvunjiko wa ndoa yake.[6]
Kuhusu usagaji nchini Nigeria, alieleza kuwa anapingana na kitendo hicho, haswa kwa sababu “Utamaduni wetu unakataza. Ni dhambi na si kitu halali. Kwa sababu gani mwanamke awe na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine?”[2]
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- Sincerity (2009)
- Secret Code
- Heart of a Widow
- Holy Serpent (with Kenneth Okonkwo)[2] (2011)
- Royal Vampire
- Palace of Vampire
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ admin (Februari 4, 2017). "I'll sue Kemi Olunloyo if she accuses me unjustly again –Angela Okorie". Punch Newspaper.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Ayinla-Olasunkanmi, Dupe (Januari 25, 2014). "Why my husband can't cheat on me–Nollywood actress Angela Okorie". Nation Newspaper.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 Ayomide, Tayo (Agosti 17, 2015). "Angela Okorie is a year older". Pulse Nigeria. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-22. Iliwekwa mnamo 2020-10-31.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Amagiya, Florence (Februari 15, 2014). "It' s not enough to get married to a rich man—Angela Okorie". Vanguard Newspaper.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Adunni, Amodeni (2016). "Full List Of Winners At City People Awards 2015". Naij.com.
- ↑ Ogbeche, Daneilla (Juni 13, 2016). "Angela Okorie opens up on alleged marriage crash". Dailypost Nigeria.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)