Genevieve Nnaji
Genevieve Nnaji | |
---|---|
![]() Genevieve Nnaji akiwa katika muda wa chakula cha mchana kwenye studio ya masuala ya mavazi ya St. Genevieve mjini Lagos Nigeria, Mei 2008 |
|
Amezaliwa | Genevieve Nnaji 3 Mei 1979 Mbaise, Imo, Nigeria |
Kazi yake | Mwigizaji, Mwanamitindo, Mwimbaji |
Genevieve Nnaji (amezaliwa tar. 3 Mei 1979 mjini Mbaise, Imo, Nigeria)[1] ni mwigizaji wa filamu na mwanamitindo kutoka nchini Nigeria. Mnamo mwaka wa 2005, ameshinda tuzo ya African Movie Academy Award - akiwa kama mwigizaji bora filamu wa Kiafrika.
Wasifu[hariri | hariri chanzo]
Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]
Genevieve Nnaji alikulia mjini Lagos. Yeye ni wa nne kuzaliwa kutoka katika familia ya watoto wanane, alikulia katika mazingira ya hali ya kawaida tu. Baba yake anafanyakazi kama mhandisi na mama yake hufanyakazi kama mwalimu. Alihitimu chuo cha Methodist Girls College Yaba, kabla kuelekeza zake katika Chuo Kikuu cha Lagos. Akiwa chuo kikuu, Genevieve alianza usaili wa shughuli za uigizaji ambazo nyingi zilikuwa kazi za Nollywood.
Shughuli[hariri | hariri chanzo]
Nnaji alianza shughuli zake za uigizaji akiwa kama mwigizaji mtoto kwenye tamthilia za televisheni – Ripples akiwa na umri wa miaka 8. Pia amewahi kushirikishwa kwenye matangazo ya biashara kadhaa ikiwemo kinywaji cha Pronto na sabuni ya Omo. Mnamo mwaka wa 1998 akiwa na umri wa miaka 19 alianza kuonekana katika soko la filamu za watu wakubwa za Kinigeria – “Most Wanted”.
Filamu zake za baadaye ni pamoja na Last Party, Mark of the Beast na Ijele.
Nnaji amepokea tuzo kadhaa kwa ajili ya kazi yake. Tuzzo hizo ni pamoja na kuopewa na jina la mwigizaji bora wa mwaka wa 2001 na City People Awards, na kupkea heshima ya kuwa mwigizaji bora mnamo mwaka wa 2005 kwenye African Movie Academy Awards (AMAA).
Mnamo mwaka wa 2004 ameingia mkataba na studio ya Kighana na kutoa albamu. Mnamo mwaka wa 2008, Nnaji ameanzisha mradi wa mavazi, "St. Genevieve," ambao pia huchangia asilia kadhaa katika mradi wa maendeleo ya uhisani.
Filmografia[hariri | hariri chanzo]
|
|