Angela Damas
Angela S. Damas (alizaliwa 16 Februari 1982) alikuwa Mrembo wa Tanzania kwa mwaka wa 2002.
Angela alizaliwa mjini Kieve nchini Ukraine. Akahamia Tanzania na baba yake ambaye ni Mjita kabila litokelealo mkoani Mara, katika wiliaya ya Musoma, Tanzania. Angela alisomea Tanzania na kisha akajiunga na masomo ya Chuo Kikuu, wakati anatwaaja taji la Mrembo wa Tanzania alikuwa ndio anaingia mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea masomo ya elimu jamii.
Angela amekuwa katika harakati mbalimbali za kijamii ambazo alianza kujishughulisha nazo tokea akiwa katika elimu ya sekondari. Angela alianza elimu yake ya chekechekea nchini Ukraine, na baada ya hapo kuendelea nchini Tanzania alipohamia na baba yake. Nchini Tanzania, Angela alianza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Kisiwandui iliyopo Zanzibar, halafu kuhamia shule ya msingi Kawe iliyopo Dar es salaam akiwa darasa la pili. Angela alisoma elimu yake ya sekondari katika shule ya sekondari ya Makongo [1], na kumalizia high school katika shule ya sekondari ya Zanaki, zote zipo jijini Dar es salaam, Tanzania.
Tokea akiwa shule, Angela amejulikana kama msichana aliyekazania masomo na pia kujihusisha sana katika shughuli za ziada za shuleni mojawapo zikiwa ni debates, na michecho, hususani mchezo wa mpira wa kikapu. Angela aliendelea na masomo yake ya Chuo kikuu katika chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo alihitimu mwaka 2005 akipata shahada ya kwanza ya masomo ya Sayansi ya jamii.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Angela Damas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |