Nenda kwa yaliyomo

Andrey Urnov

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Andrey Yuryevich Urnov (kwa Kirusi Андрей Юрьевич Урнов; amezaliwa Moscow, 10 Novemba 1937) ni mwanadiplomasia wa Umoja wa Kisovyeti na Urusi, daktari wa historia na kaka mkubwa wa mchumi na mtaalamu wa siasa Mark Urnov[1].

Baada ya kaka yake mdogo Mark kuzaliwa mama yake aliyekuwa mwigizaji wa Thieta ya Jeshi la Kisovyeti alibadilisha kazi na kuanza kufundisha katika Chuo Kikuu cha Sanaa ya Maonyesho cha Shchepkin. Baba yake Yuri Kushnir alijishughulisha darubuni za vidudu za umeme kwenye taasisi ya siri na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alieneza propaganda kati ya maadui katika mstari wa mapigano[2].

Babu yake wa kuumeni Mark Kushnir alikuwa mpasuaji na mwanachama wa zamani wa Chama cha Demokrasia. Babu wa kuukeni Vasily Urnov mwenye asili yake ya wakulima alikuwa mwalimu wa shuleni, mwanachama wa Chama cha Mapinduzi ya Kijamii na mwenyekiti wa Kamati ya Wanajeshi ya Moscow mwaka 1917[3].

Mwaka 1961 Andrey Urnov alihitimu katika Chuo Kikuu cha Moscow cha Mahusiano ya Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Kisovyeti (MGIMO).

Alikuwa makamu wa mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti.

Tangu mwaka 1990 anafanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi. Kuanzia tarehe 15 Agosti 1990 hadi tarehe 5 Julai 1994 alikuwa balozi wa Umoja wa Kisovyeti / Shirikisho la Urusi nchini Namibia[4].

Tangu tarehe 13 Septemba 1994 hadi tarehe 12 Novemba 1998 alikuwa balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Armenia.

Kuanzia Desemba mwaka 1998 alikuwa naibu mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Maeneo ya Shirikisho, Bunge na Mashirika ya Kijamii na Kisiasa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Urusi.

Miaka 1999-2000 alikuwa mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Maeneo ya Shirikisho, Bunge na Mashirika ya Kijamii na Kisiasa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Urusi.

Sasa ana kiti cha mjumbe maalumu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Urusi. Pia anaongoza Tume ya Kikazi ya Urusi juu ya Hadhi ya Bahari ya Kaspi.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Ameoa na ana watoto wawili wa kiume.

Maandishi makuu

[hariri | hariri chanzo]
  • Юг Африки — новый этап освободительной борьбы // Международный ежегодник. Политика и экономика, М., 1977 (псевд. А. Рунов).
  • Политика ЮАР в Африке, М., 1982;
  • Белый дом и чёрный континент, М, 1984 (в соавт.);
  • South Africa Against Africa (1966-1986). Progress Publishers, 1988;
  • Африка и ООН на исходе первого десятилетия XXI века. М., 2011;
  • Внешняя политика СССР в годы «холодной войны» и «нового мышления». М., 2014;
  • США и Африка: политика администрации Б. Обамы (2009-2014). М., 2015.
  1. "Валерия Касамара делит декана «Вышки» с законной женой". EG.RU (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 2024-01-14. EG.RU. Iliwekwa mnamo 2024-01-14.
  2. "Интервью с Марком Урновым | Ельцин Центр". www.yeltsincenter.ru. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-14. Iliwekwa mnamo 2024-01-14. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help) www.yeltsincenter.ru. Iliwekwa mnamo 2024-01-14.
  3. Литература как жизнь. Том I. Дмитрий Урнов. Издательство им. Сабашниковых, 2021. ISBN 978-5-82-420178-9
  4. "Справочник по истории Коммунистической партии и Советского Союза 1898—1991". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2008-10-08. {{cite web}}: Unknown parameter |deadlink= ignored (|url-status= suggested) (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]