Nenda kwa yaliyomo

Ananda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya kuchonga kutoka Java inawaonyesha Buddha na Ananda

Ananda (karne ya 54 KK) alikuwa mhudumu mkuu wa Buddha na mmoja wa wanafunzi wake wakuu kumi. Miongoni mwa wanafunzi wengi wa Buddha, Ananda anaheshimiwa hasa kwa kuwa na kumbukumbu bora zaidi. Hivyo mafundisho mengi ya Buddha ambayo yamehifadhiwa katika maandiko ya Sutta-Piṭaka (Pāli; Sanskrit Sutra-Pitaka) yanategemea kukumbuka kwake. Kwa sababu hiyo, anaheshimiwa kama Mweka Hazina wa Dhamma, wakati Dhamma (Kisanskrit: dharma) inamaanisha mafundisho ya Buddha.

Sehemu ya mapokeo inasema kwamba Ananda alikuwa binamu wa Buddha. Alitawazwa kuwa mtawa na Puṇṇa Mantānīputta akawa mwalimu wake. Baadaye Buddha alimchagua kuwa mhudumu wake.

Aliandamana na Buddha kwa maisha yake yote, akitenda sio tu kama msaidizi, bali pia katibu na msemaji wake.

Ānanda ni mmoja wa watu wanaopendwa sana katika Ubuddha. Alijulikana kwa kumbukumbu yake, elimu na huruma, na mara nyingi alisifiwa na Buddha kwa mambo haya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Baruah, Bibhuti (2000), Buddhist Sects and Sectarianism (PDF), Sarup & Sons, ISBN 9788176251525, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 14 Septemba 2018{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Princeton Dictionary of Buddhism Princeton University Press 2018, ISBN 978-0-691-15786-3]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]