Buibui-mjeledi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Amblypygi)
Jump to navigation Jump to search
Buibui-mjeledi
Buibui-mjeledi akionyesha pedipalpi na mijeledi
Buibui-mjeledi akionyesha pedipalpi na mijeledi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Oda: Amblypygi
Ngazi za chini

Familia 5:

Buibui-mjeledi (kutoka Kiing. whip spider) ni arithropodi wa oda Amblypygi katika ngeli Arachnida wafananao na buibui wa kawaida. Kama hawa wana miguu minane lakini hawawezi kusokota nyuzi za hariri. Kiwiliwili chao kina sehemu mbili kama buibui: kefalotoraksi (cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio zilizoungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija. Mgongo wa kefalotoraksi ni ngumu na kwa hivyo huitwa gamba (carapace). Kinyume na buibui kelisera (chelicerae) za buibui-mjeledi ni fupi na pedipalpi ni ndefu zenye gando kama kaa. Pedipalpi hutumika kwa kukamata mawindo na kelisera kwa kuyakatakata. Miguu sita tu hutumika kwa kutembea. Jozi ya kwanza imekuwa miembamba na mirefu sana mpaka zaidi ya mara nne urefu wa mwili (inafanana na mijeledi, asili ya jina lao) na hutumika kama vipapasio. Buibui-mjeledi hula arithropodi wengine.

Picha[hariri | hariri chanzo]

WikiLettreMini.svg Makala hii kuhusu "Buibui-mjeledi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili whip spider kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni buibui-mjeledi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.