Amando na Juniano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Amando na Juniano (karne ya 5 - karne ya 6) walikuwa wakaapweke karibu na Limoges, katika Ufaransa wa leo[1].

Amando alihamia huko ili kuishi kitawa akitokea labda Hungaria. Askofu alimkubali. Kabla hajafa alimpokea mvulana Juniano kama mwanafunzi, naye aliendeleza kwa miaka 40 mtindo wa maisha wa Amando akapata sifa kubwa zaidi hata upande wa miujiza.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Oktoba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/74215
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.