Alvaro Negredo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Alvaro Negredo

Alvaro Negredo Sanchez (amezaliwa Madrid, Hispania, 20 Agosti 1985) ni Mhispania mchezaji wa soka katika timu ya Al Nasri ya Uarabuni.

Alvaro Negredo Sanchez Kwa jina la utani Anaitwa La fiera de Vallecas yaani (Mnyama wa Vallecas). Alvaro Negredo Amechezea Rayo Vallecano, Real Madrid B, Almería, Real Madrid, Sevilla, Manchester City, Valencia, Middlesbrough, Beşiktaş na Sasa Al-Nasr. Katika misimu minane ya La Liga, alipata kucheza jumla ya mechi 264 huku akifunga mabao 112. Negredo alipata kucheza michezo 21 kwa timu ya Taifa ya Uhispania, akifunga mabao kumi, kati ya 2009 na 2013, na alikuwa sehemu ya timu ambayo ilishinda Euro 2012.

Mwanzoni kwa mwaka 2005 Alvaro Negredo alijiunga na klabu ya Real Madrid B ambayo ilikuwa inashiriki ligi daraja la pili kwa wakati huo Negredo alionyesha uwezo mkubwa mpaka kwaka 2007 alifikisha jumla ya magoli 22 katika michezo 65 licha ya kuonyesha uwezo huo Negredo alijiunga na timu ya Almeria mwaka huo 2007 na kufanikiwa kucheza michezo 70 na kufunga mabao 32 ndipo kwaka 2009 akapata nafasi ya kujiunga na klabu ya Real Madrid lakini kocha wa Real Madrid kwa wakati huo Manuel Pellegrini hakuona umuhimu wa kumtumia Negredo kwani alikuwa anawashambuliaji kama Clistian Ronaldo,Karim Benzema,Raul pamoja na Raud Van Nestroy ndipo alipouzwa Sevilla kwa paundi milioni 15 akiwa ajacheza mchezo wowote wa Real Madrid.

Akiwa Sevilla alifanikiwa kucheza michezo 139 na kufanikiwa kuifungia Sevilla mabao 70 ndipo alipojiunga na klabu ya Manchester City mwaka 2013 lakini mwaka 2014 alipelekwa kwa mkopo klabu ya Valencia mwisho akauzwa moja kwa Moja kuichezea Valencia mwaka 2015 hata hivyo mwaka 2016 Alijiunga na klabu ya Middlessburg kwa mkopo na mwaka 2017 akajiunga klabu ya Uturuki Besiktas hakukaa sana klabuni hapo ndipo akajiunga na klabu ya Al Nasri.

Alvaro Negredo, ana ndugu wawili wa kiume ambao Ni César na Rubén, hawa wote pia walikuwa ni wachezaji wa mpira wa miguu, mmoja alikuwa ni mlinzi na wa pili mshambuliaji.

Baba yake, Alvaro Negredo José María, alifanya kazi kama dereva wa teksi huko Madrid.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alvaro Negredo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.