Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (ing. International Phonetic Alphabet, kifupi IPA) ni mfumo wa alfabeti inayolenga kuonyesha sauti za lugha zote duniani. Imetungwa na wataalamu wa isimu wanaoshirikiana katika Shirika ya Kimataifa ya Fonetiki (International Phonetic Association). Inatumiwa na watunga kamusi, walimu na wanafunzi wa lugha za kigeni, wanaisimu na wafasiri kote duniani. Kwa hiyo tunakuta alama zake katika kamusi na mara yningi pia kwenye makala za wikipedia.

Msingi wa IPA ni alfabeti ya Kilatini pamoja na herufi za pekee zilizochukuliwa kutoka alfabeti nyingine. Herufi hizi zinaunganishwa na alama za pekee.

Mfano ni alama zinazoonyesha sauti tofauti ambazo mara nyingi zinaonyeshwa kwa herufi "A" ambazo zinaweza kuwa na sauti tofauti katika lugha na lahaja mbalimbali kama vile a Loudspeaker.png  ? , ɐLoudspeaker.png  ?, ɑ Loudspeaker.png  ?, ɒ Loudspeaker.png  ?, æ Loudspeaker.png  ?, ɑ̃ au ʌ Loudspeaker.png  ? (boyfa pembetatu ndogo kwa kusikia sauti).

Orodha ya alama zote za IPA pamoja na sauti inapatikana katika wikipedia ya Kijerumani hapa

Tangu masahihisho ya mwaka 2005 kuna herufi 107 na alama za pekee 56.