Alexander von Humboldt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Alexander von Humboldt alivyochorwa na Joseph Stieler 1843

Friedrich Wilhelm Heinrich Alexander Freiherr von Humboldt (14 Septemba 17696 Mei 1859) alikuwa mpelelezi na mwanasayansi kutoka Prussia katika Ujerumani. Kaka yake alikuwa waziri wa elimu wa Prussia na mtaalamu wa lugha.

Alexander alifanya utafiti muhimu katika jiografia na biolojia.

Humboldt alizaliwa mjini Berlin. Babake Alexander Georg von Humboldt alikuwa mwanajeshi wa Prussia. Akiwa mtoto Alexander alipenda kukusanya mimea, konokono na wadudu.

Kati ya 1799 na 1804 Humboldt alisafiri katika Amerika ya Kusini akiwa mwanasayansi wa kwanza wa kuandika juu ya safari yake katika maeneo haya. Alitambua tayari ya kwamba Amerika Kusini na Afrika ziliwahi kuwa bara ya pamoja kutokana na aina za mimea na wanyama zilizofanana pande zote mbili.

Baadaye aliongeza safari ya kutembelea Asia ya Kati na sehemu kubwa ya muda wake alitumia kuandika taarifa ya safari hizi na kufanya utathmini ya yale aliyoona na kukuta. Alijaribu kukusanya ujuzi wote wa sayansi wa wakati wake katika "Kosmos" iliyokuwa aina ya kamusi elezo yenye vitabu vitano.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]