Alan H. Borning

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alan H. Borning ni mwanasayansi wa kompyuta wa Marekani aliyejulikana kwa utafiti wake kuhusu mwingiliano wa kompyuta na binadamu na utengenezaji wa programu zinazolenga kitu . Utafiti wake ulilenga mwingiliano wa binadamu na kompyuta na juu ya kubuni bahadhi ya programu zinazoipa kompyuta thamani kwa mwanadamu. [1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Borning alipokea Shahada ya sanaa katika Hisabati kutoka Chuo cha Reed mnamo 1971. Alipata Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Stanford mnamo 1974 na Ph.D katika Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Stanford mnamo 1979.

Kisha alijiunga na Idara ya Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Washington mnamo 1980, ambapo mpaka 2016 alikua bado ni profesa huko. Yeye pia ni profesa msaidizi katika Shule ya Habari, na mwanachama wa Programu za uzamivu katika Usanifu wa Miji na Mipango.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2001, alikua Mshirika wa ACM [2] kwa michango wke kwa lugha na utengenezaji wa mifumo inayolenga kuelewa masuala ya kompyuta na jamii.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Cassowary linear arithmetic constraint solving algorithm, Authors: Greg J. Badros, Alan Borning & Peter J. Stuckey
  2. Association of Computing Machinery (2014-07-01). "ACM Awards ACM Fellow". ACM. Iliwekwa mnamo 2014-07-01. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]