Nenda kwa yaliyomo

Akua Asabea Ayisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akua Asabea Ayisi
Amezaliwa 3 Aprili 1927
Mampong Akwapem
Nchi Ghana
Kazi yake Mwanahabari

Akua Asabea Ayisi (3 Aprili 1927 - 21 Aprili 2010) alikuwa mpenda maendeleo ya wanawake, Jaji wa zamani wa Mahakama Kuu na mwanahabari wa kwanza mwanamke kutoka Ghana. [1] Wakati wa kuibuka kwa vuguvugu la kupigania uhuru wa Ghana, Akua Asabea Ayisi alifunzwa kama mwandishi wa habari na Mabel Dove-Danquah na Kwame Nkrumah, ambaye baadaye alikuwa waziri mkuu na Rais wa kwanza wa nchi.

Nafasi ya Ayisi kama mhariri wa safu ya wanawake, ambayo iliangazia masuala ya wanawake, katika gazeti la Accra Evening News ilionekana ni hatua kubwa kwa wakati huo. [2]

Familia na Maisha

[hariri | hariri chanzo]

Akua Asabea Ayisi alizaliwa tarehe 3 Aprili 1927, huko Mampong Akwapem na alikuwa mtoto wa nane kati ya kumi kwa wazazi wao Mercy Adebra Mensah na Okyeame Kofi Ayisi.

Kofi Ayisi alikuwa mwanaisimu (mtaalamu wa lugha) wa Mfalme, pia alikuwa jamaa yake na mfalme. Baadhi ya wajomba zake Akua Asabea Ayisi walikuwa waganga wa kifalme. Kofi Ayisi alikuwa na watoto 70, Mercy Adebra alikuwa na 10 kati ya hao. Mamake Ayisi, babu yake Mercy Adebra, Tetteh Quarshie alipanda mti wa kwanza wa kakao nchini Ghana. Mercy Adebra, mwanamke shupavu aliyetaka kujitegemea, hatimaye alimwacha Kofi Ayisi na kuhamia Accra kuwa karibu na familia yake iliyokuwa Gas . [3]

  1. Tuntum Nahana, Akosua (9 Februari 2019). "Ghana's first female journalist Akua Asabea Ayisi". modernghana.com. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Kwarteng, Francis. "Mabel Dove-Danquah: A Trailblazing Author, Feminist, Politician, Activist & Journalist", Modern Ghana. 
  3. Contributor, Akosua Tuntum Nahana News. "Ghana's first female journalist Akua Asabea Ayisi". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-04-07. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akua Asabea Ayisi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.