Nenda kwa yaliyomo

Acamprosate

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Acamprosate
Skeletal formula of acamprosate
Ball-and-stick model of the acamprosate molecule
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
3-Acetamidopropane-1-sulfonic acid
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Campral, Aotal, mengineyo[1]
AHFS/Drugs.com Monograph
Kategoria ya ujauzito C[2] (US) B2 (AU)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo[2]
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili 11%[2]
Kufunga kwa protini Kunapuuzika[2]
Kimetaboliki Hakuna[2]
Nusu uhai Masaa 20 hadi 33 [2]
Utoaji wa uchafu Figo[2]
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe N-Acetyl homotaurine
Data ya kikemikali
Fomyula C5H11NO4S 
 N(hii ni nini?)  (thibitisha)

Acamprosate, inayouzwa kwa jina la chapa Campral miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumiwa pamoja na ushauri nasaha kutibu utegemezi wa pombe.[1] Inapotumiwa peke yake, haina ufanisi kwa watu wengi;[3] inafanya kazi vyema zaidi inapotumiwa pamoja na ushauri nasaha.[1][4] Inachukuliwa kwa mdomo.[5]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara na udhaifu.[6] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha athari za mzio, mabadiliko ya hisia, mawazo ya kujiua na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.[7] Kiwango cha chini kinapendekezwa kwa watu walio na matatizo madogo ya figo na matumizi yake hayapendekezi kwa watu wenye ugonjwa mkali wa figo.[6] Matumizi yake ni sawa katika hali ya kutofanya kazi kwa ini kwa chini hadi wastani.[8] Usalama wake wakati wa ujauzito haueleweki.[9] Acamprosate inadhaniwa kufanya kazi kwa kubadilisha ishara za kemikali kwenye ubongo.[8]

Acamprosate iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2004[6] na iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[10] Inapatikana kama dawa ya kawaida nchini Uingereza ambapo mwezi mmoja wa matumizi yake uligharimu NHS kama pauni 30 kufikia mwaka wa 2020.[5] Kiasi hiki nchini Marekani kiligharimu kama dola 80 za Marekani kufikia mwaka wa 2020.[11]

  1. 1.0 1.1 1.2 Plosker, GL (Julai 2015). "Acamprosate: A Review of Its Use in Alcohol Dependence". Drugs. 75 (11): 1255–68. doi:10.1007/s40265-015-0423-9. PMID 26084940.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Campral label" (PDF). FDA. Januari 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 27 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) For label updates see FDA index page for NDA 021431 Archived 2021-08-27 at the Wayback Machine
  3. Malenka RC, Nestler EJ, Hyman SE, Holtzman DM (2015). "Chapter 16: Reinforcement and Addictive Disorders". Molecular Neuropharmacology: A Foundation for Clinical Neuroscience (tol. la 3rd). New York: McGraw-Hill Medical. ISBN 9780071827706. Unfortunately, acamprosate is not adequately effective for most alcoholics.
  4. Nutt, DJ (2014). "Doing it by numbers: A simple approach to reducing the harms of alcohol". Journal of Psychopharmacology. 28 (1): 3–7. doi:10.1177/0269881113512038. PMID 24399337. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-27. Iliwekwa mnamo 2020-01-22.
  5. 5.0 5.1 BNF 79 : March 2020. London: Royal Pharmaceutical Society. 2020. uk. 509. ISBN 9780857113658.
  6. 6.0 6.1 6.2 "Acamprosate Calcium Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Acamprosate". drugs.com. 2005-03-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2006. Iliwekwa mnamo 2007-01-08.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 Williams, SH. (2005). "Medications for treating alcohol dependence". American Family Physician. 72 (9): 1775–1780. PMID 16300039. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-29. Iliwekwa mnamo 2006-11-29.
  9. "Acamprosate (Campral) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. World Health Organization (2023). The selection and use of essential medicines 2023: web annex A: World Health Organization model list of essential medicines: 23rd list (2023). Geneva: World Health Organization. hdl:10665/371090. WHO/MHP/HPS/EML/2023.02.
  11. "Acamprosate Prices, Coupons & Savings Tips". GoodRx (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Septemba 2016. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)