2Africa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

2Africa ni kebo ya baharini ya mawasiliano ya kimataifa ambayo huzunguka ufuo wa Afrika chini ya uso wa bahari ili kuiunganisha Afrika na Ulaya, Mashariki ya Kati na Uhindi[1]. Inagharamiwa na ushirikiano unaojumuisha kampuni za simu kadhaa pamoja na Meta. Mfumo huo utakuwa wa kwanza kutumia :en:Spatial multiplexing (SDM1). [2] [3]

Kebo ya 2Afrika inaanza Ulaya ikipitia Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Hindi, na kisha kurudi Ulaya kupitia Bahari ya Shamu na Bahari ya Mediteranea . [4]

2Afrika ni kebo ndefu duniani inayowekwa kwenye tako la bahari. Inaunganisha vituo 46 katika nchi 33 za Afrika, Asia na Ulaya ikiwa na urefu wa kilomita 45,000. Kebo ya 2Africa ina uwezo wa kubeba hadi tbps 180 ukitumia jozi 16 za nyuzi badala ya jozi 8 zilizokuwa kawaida.[5]

Marejeo

  1. Airtel to Land 2Africa Pearls in Mumbai, India , tovuti ya submarinenetworks.com ya tarehe 15 Desemba 2022
  2. Facebook to build a subsea cable to improve connectivity in Africa, tovuti ya zdnet.com ya Mei 2020
  3. Vermeulen, Jan (9 December 2022). "Facebook’s massive undersea cable lands in South Africa". MyBroadband. Iliwekwa mnamo 9 December 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. Chanthadavong, Aimee. "Facebook to build a subsea cable to improve connectivity in Africa". ZDNet (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-05-15. 
  5. https://www.businesswire.com/news/home/20200514005389/en/2Africa-A-Transformative-Subsea-Cable-for-Future-Internet-Connectivity-in-Africa-Announced-by-Global-and-African-Partners 2Africa: A Transformative Subsea Cable for Future Internet Connectivity in Africa Announced by Global and African Partners, tovuti ya businesswire.com, iliangaliwa Machi 2023

Viungo vya nje