Meta Platforms

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

 

Logo ya Meta

Meta Platforms, Inc. ni kampuni ya intaneti inayojulikana kwa kifupi chake Meta. Kabla ya mwaka 2021 ilifahamika kama Facebook, kampuni lililomilikiwa na Mark Zuckerberg pamoja na waanzilishi wengine na wafanyakazi wake. Makao makuu yako California, Marekani.

Tangu Februari 2012 kampuni ilianza kutoa hisa hadharani.

Pamoja na mtandao wa kijamii Facebook, Meta inamiliki huduma za Instagram, WhatsApp, Messenger na Meta Quest. Kwenye mwaka 2021 kampuni ya Meta ilipata asilimia 97.5 ya mapato yake kutokana na kuuza nafasi za matangazo yanayowekwa na kampuni nyingine kwenye kurasa za huduma zake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]