Yefta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yefta alivyochorwa katika Promptuarii Iconum Insigniorum ya Guillaume Rouillé.
Binti Yefta, mchoro wa Alexandre Cabanel (1879).

Yefta (kwa Kiebrania יפתח‎‎, Yip̄tāḥ) alikuwa mmojawapo kati ya Waamuzi wa Biblia.

Kadiri ya Waamuzi 11-12 alikuwa wa kabila la Manase au wa kabila la Gadi akaongoza Israeli kwa miaka 6[1].

Alikuwa na mtoto mmoja tu, tena wa kike[2], lakini alimtoa sadaka kwa Mungu kama shukrani kwa kumpa ushindi vitani dhidi ya Waamoni. Alifanya hivyo ili kutimiza nadhiri aliyoweka kwanza, bila kujua kwamba Torati inakataza sadaka za namna hiyo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yefta kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.