William Berger
William Thomas Berger (20 Januari 1928 mjini Innsbruck, Austria – 2 Oktoba 1993 ndani ya Los Angeles, Marekani, kwa ugonjwa wa Kansa) alikuwa muigizaji filamu wa kiulaya, alishiriki zaidi katika filamu za Ulaya au zile za spaghetti westerns na dokumentali za safari.
Shughuli za Mwanzo
[hariri | hariri chanzo]Kazi yake mwanzo kabisa ilikua katika kampuni ya uundaji wa filamu, maarufu kama Broadway theater. Kuna kipindi alifanya matembezi kadha wa kadha huko nchini Italia, ndio ikawa mara yake ya kwanza kushiriki katika filamu za western, filamu hiyo ilikuwa inaitwa Break Up ilichezwa mnamo 1965. Kuanzia hapo ndiyo akaanza filamu za westerns kwa mtindo wa mfululizo.
Miongoni mwa filamu hizo ni kama ifuatavyo: Faccia a faccia (1967), If You Meet Sartana Pray for Your Death (1968), The Sabata Trilogy (1969) na Keoma (1975).
Kwenye miaka ya 1970 hivi, Berger alitumikia kifungo kidogo katika jela za Kiitalia, alishtakiwa kwa kosa la kumiliki bangi na madawa ya kulevya, kwa bahati nzuri alirudia shughuli zake za uigizaji baada ya kutoka.
Kazi alizofanya baadaye ilibeba filamu, Hercules (1983), Devil Fish (1984), The Brother from Space (1988), Dial Help (1988) na The King's Whore (1990).