Nenda kwa yaliyomo

Vision of Love

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Vision of Love”
“Vision of Love” cover
Single ya Mariah Carey
kutoka katika albamu ya Mariah Carey
B-side "Sent From Up Above"
Imetolewa Mei 15, 1990 (1990-05-15)
Muundo CD single, cassette single, 7" single
Imerekodiwa Januari 1989
Aina Pop, R&B
Urefu 3:31
Studio Columbia
Mtunzi Mariah Carey, Ben Margulies
Mtayarishaji Rhett Lawrence, Narada Michael Walden
Certification Gold (Australia, New Zealand, U.S.)

"Vision of Love" ni wimbo wenye miondoko ya pop na R&B ulioandikwa na Mariah Carey akishirikiana na Ben Margulies na kutayarishwa na Rhett Lawrence pamoja na Narada Michael kwa ajili ya albamu ya Mariah Carey iliyoitwa Mariah Carey iliyaotoka rasmi mwaka 1990. Wimbo huu ulitoka kama single ya pili katika mwaka 1990, nchini Marekani na na baadae mwaka huo huo ilitoka katika maeneo mrngine ya dunia. Wimbo huu ulifanikiwa kukaa katika nafasi ya kwanza katika chati ya Billboard Hot 100 kwa wiki nne mfululizo.

Historia ya wimbo

[hariri | hariri chanzo]

Vision of Love ni wimbo wa kwanza kuandikwa na Carey akishirikiana na Margulies mara baada tu ya Carey kusaini mkataba waka na studio za Columbia Rocords chini ya mkurugenzi wake Tommy Mottola. Miondoko ya albamu hii imetungwa na Carey kwa kushirikiana na Margulies ambayo kwa kiasi fulani huweza kufanana na ile ya miaka ya 1950 [1].

Wadadisi wa mambo wanadai kuwa, wimbo wa vision of love unaelekea kushukuru upendo kwa Mungu zaidi kuliko upendo kwa mpenzi. Mashairi katika wimbo huu yanaelekea kuonesha ndoto za Mariah kuwa mwanamuziki..[2] Carey aliliambia gazti la Ebony kuwa, wimbo huu unaelezea kila kitu kuhusu maisha yangu. Kwa mujibu wake anasema kuwa, mashairi ya wimbo huu yanaeleze harakati zake za binafsi alipokuwa mdogo, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na kutengana kwa wazazi wake pamoja na uhusiano kati y familia yao na majirani zao.[3] Carey's vocal range in the song is Eb3-C7.

Mapokezi

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo huu ulichaguliwa kugombea tuzo ya Grammy Awards za mwaka 1991, katika jamii ya mwanamke mwenye sauti nzuri, ambapo wimbo huu ulishinda, na pia Tuzo kwa ajili ya wimbo bora wa mwaka [4] .


Jarida la Entertainment Weekly la mwaka 2005, liliandika kuwa wimbo wa Mariah Carey unavutia hususani kwa wale waimbaji wa wadogo. ."[5]

Nchini Marekani, wimbo wa ‘’’Vision of Love’’’ uliingia katika chati za Billboard Hot 100 na kufikia katika nafasi ya 73, hii ikiwa ni tarehe 2 Juni 1990, na uliweza kufikia katika nafasi ya kwanza katika wiki yake ya tisa.[6] Single hii ilifika katika nafasi ya kwanza katika chati ya Hot R&B/Hip-Hop Songs kwa muda wa wiki mbili, na katika chati ya Hot Adult Contemporary Tracks kwa wiki tatu. Wimbo wa "Vision of Love" uliingia katika nyimbo kumi bora nchini Australia, Ufalme wa Muungano, Ireland na Uholanzi na kufanikiwa kufika katika nafasi ya kwanza nchini Kanada na New Zealand.

Waliourudia

[hariri | hariri chanzo]
  • Christina Aguilera aliurudia wimbo huu akiwa na miaka kumi..
  • Lara Fabian aliuimba wimbo huu katika tamasha lake lililofanyika katika eneo la Sonia Benezra.
  • Jane Zhang aliuimba wimbo huu katika tamasha lake la Super Girl.
  • Kyla aliuimba wimbo huu katika tamasha lake lililofanyika nchini Philippines.

Orodha ya nyimbo na muundo

[hariri | hariri chanzo]

CD iliyotoka kwa ajili ya ulimwengu mzimae[7]

  1. "Vision of Love"
  2. Special excerpts from the debut release "Prisoner/All in Your Mind/Someday"

UK CD single[8]

  1. "Vision of Love"
  2. "Sent from Up Above"

UK CD maxi-single

  1. "Vision of Love"
  2. "Sent from Up Above"
  3. Special excerpts from the debut release "Prisoner/All in Your Mind/Someday"
Chati (1990) Ilipata
nafasi
Australian Singles Chart[9] 9
Canadian Singles Chart[10] 1
Dutch Singles Chart[11] 8
French Singles Chart[12] 25
German Singles Chart[13] 17
Irish Singles Chart[14] 10
New Zealand Singles Chart[15] 1
Swedish Singles Chart[16] 17
Swiss Singles Chart[17] 24
UK Singles Chart[18] 9
U.S. Billboard Hot 100[19] 1
U.S. Billboard Hot Adult Contemporary Tracks[19] 1
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs[19] 1

Wasambazaji Mauzo Certification
Australia 35,000+ Gold
New Zealand 7,500+ Gold
United States 500,000+ Gold
  1. Hogan, Ed. "Vision of Love - Mariah Carey - Song Review". Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-08-30. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  2. "Pop's New Vision", Rolling Stone, 28 Mei 1990
  3. Norent, Lynn (Machi 1991), "Mariah Carey: 'Not another White girl trying to sing Black.'", Ebony, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-05-29, iliwekwa mnamo 2010-01-27 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. "Mariah Carey". ARC Weekly Top 40. Iliwekwa mnamo 2008-08-30. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  5. Slezak, Michael (15 Desemba 2005). "Gem Carey". EW.com. Entertainment Weekly and Time Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-07. Iliwekwa mnamo 2008-08-30. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help); Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  6. Bronson, Fred (2003), The Billboard Book of Number 1 Hits (tol. la 5th), Billboard Books, ISBN 0823076776, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-22, iliwekwa mnamo 2010-01-27 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  7. "Discogs". Mariah Carey - Vision of Love (12") at Discogs. Iliwekwa mnamo 1990. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  8. "EIL.com". Mariah Carey Vision of Love UK 7" RECORD (30802). Iliwekwa mnamo 1990. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  9. Australian Singles Chart
  10. Canadian Singles Chart
  11. Dutch Singles Chart
  12. French Singles Chart
  13. German Singles Chart
  14. Irish Singles Chart
  15. "New Zealand Singles Chart". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-21. Iliwekwa mnamo 2010-01-27. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://www.webcitation.org/5wChHAS9r?url= ignored (help)
  16. Swedish Singles Chart
  17. Swiss Singles Chart
  18. UK Singles Chart
  19. 19.0 19.1 19.2 "Artist Chart History - Mariah Carey". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-04. Iliwekwa mnamo 2008-04-04.