Veto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Veto (Kilatini "ninakataa") ni haki ya kukataza azimio hata kama limetolewa na wengi.

Yaliyomo

[hariri] Veto ya rais dhidi ya bunge

Katika nchi nyingi rais au kiongozi wa taifa ana haki ya kukataza maazimio au sheria zilizokubaliwa na bunge akiona kasoro au hasara ndani yake kwa manufaa ya taifa.

Kwa mfano nchini Marekani rais ana haki ya kukataza kila sheria iliyokubaliwa na bunge katika kipindi cha siku 10 baada ya azimio la bunge. Akipiga veto sheria inarudi bungeni. Hapa bunge linaweza kufuta veto kwa theluthi mbili za kura zake au bune linaweza kubadilisha sheria hadi kupatana na mapenzi ya rais.

[hariri] Veto katika Umoja wa Mataifa

Mataifa matano yana haki ya veto katika Baraza la Usalama la UM ambayo ni China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Kila moja kati yao anaweza kuzuia maazimio ya baraza la usalama.

[hariri] Asili ya Kihistoria

Asili ya neno "veto" iko katika lugha ya Kilatini. Katika Roma ya Kale kulikuwa na afisa mmoja aliyekuwa mwakilishi wa wananchi wa kawaida mbele ya senati ya Roma. Kama maseneta ambao wote walitoka katika familia za makabaila walitoa maamuzi ya kuathiri vibaya hali ya wananchi raia huyu mwakilishi alikuwa na haki ya kupiga veto hivyo kuzuia azimio.

[hariri] Viungo vya nje