Nikolasi Saggio wa Longobardi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Nikola katika mchoro huko Campora San Giovanni.

Nikolasi Saggio wa Longobardi (kwa Kiitalia Nicola Giovanni Battista Clemente Saggio da Longobardi; Longobardi, mkoa wa Calabria, 6 Januari 1650Roma, 3 Februari 1709) alikuwa mtawa wa shirika la Waminimi nchini Italia.

Nikola anasemekana alizaliwa kwa muujiza; sehemu kubwa ya maisha yake alifanya kwa unyenyekevu na utakatifu kazi ya bawabu wa konventi ya jumuia.

Alitambuliwa na papa Pius VI kuwa mwenye heri tarehe 17 Septemba 1786, akatangazwa na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 23 Novemba 2014.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Februari[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.