Mtando chakula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa mtando chakula katika bahari ya aktiki

Mtando chakula ni neno linaloashiria uhusiano wa kilishe kati ya viumbehai mbalimbali katika mazingira fulani.

Mfano mwepesi ni: panya anayekula nafaka analiwa na nyoka; nyoka analiwa na tai; tai kwa kawaida hana adui anayemshinda lakini akifa mwili wake huliwa na sisimizi na labda tena panya mwingine. Kama mwili wake unaoza bila kuliwa unageuka tena kuwa minerali zitakazolisha mimea ambayo tena ni chakula cha panya.

Hali halisi uhusiano katika mitando ya chakula si mwepesi hivi kwa sababu kuna spishi nyingi zaidi zinazoishiriki.

Njia nyingine ya kuitazama ni jinsi nishati inapitishwa kutoka spishi moja kwenda kwa nyingine.

Karibu kila mtando chakula huanza na nguvu ya nuru ya jua; nishati hii inapokelewa na mimea kwa njia ya usanisinuru na kutumiwa kwa kujenga mwili wa mmea wenyewe. Mimea hiyo huliwa na wanyama wala majani ambao tena huliwa na wanyama wala nyama. Miili ya wanyama hao wakifa inaoza tena pamoja na sehemu za mimea ambayo hayaliwi na yote inakuja kuliwa na vijidudu vinavyoigeuza kuwa rutuba. Rutuba hii hunawilisha udongo na kuwa chakula cha mimea.

Picha katika makala hii inaonyesha sehemu ya mtando chakula katika bahari ya Aktiki:

  1. Chanzo ni nuru ya jua inayolisha
  2. Planktoni mimea (fitoplanktoni) inayolisha
  3. Planktoni wanyama (zuoplanktoni) wanaolisha
  4. Samaki wengi wadogo lakini pia aina mbalimbali za samaki wakubwa hadi [[mamalih ya nyangumi.
  5. Samaki huliwa na wanyama wengine kama ndege za bahari, sili, papa na wakati mwingine hata dubu aktiki.
  6. Sili ni chakula cha papa na dubu aktiki.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtando chakula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.