Magnesi
| Magnesi (Magnesium) |
|
|---|---|
| Jina la Elementi | Magnesi (Magnesium) |
| Namba atomia | 12 |
| Mfululizo safu | Metali za udongo alikalini |
| Uzani atomia | 24,305 u |
| Valensi | 2, 8, 2 |
| Kiwango cha kuyeyuka | 923 K (650 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 1380 K (1107 °C) |
Magnesi ni elementi na metali ya udongo alikalini yenye namba atomia 12 kwenye mfumo radidia ina uzani atomia 24.3050. Alama yake ni Mg. Jina lahusiana na neno la kigiriki μαγνησιη (magnesia - sumaku) hata kama Mg haina tabia za kisumaku.
Elementi tupu ina valensi mbili na rangi yake ni nyeupe-fedha. Mg ni kati ya elementi zinazopatiikana kwa wingi duniani ikiwa na nafasi ya nane na asilimia 1.4 za ganda la dunia ni magnesi.
Inamenyuka rahisi kikemia hivyo haitokei kama elementi tupu lakini kwa kampaundi mbalimbali hasa katika magnesiti, dolomiti na madini mengine. Katika maji ya bahari iko kwa kiwango cha kg 1 kwa kila m³.
Unga wa magnesi au vipande vidogo vya metali huungua moto mkali mweupe, unga hata bila kuwashwa hewani tu.
Magnesi ni muhimu kwa miili ya wanadamu na wanyama pia kwa mimea. Wanamichezo hutumia mara nyingi dawa la magnesi wakitaka kuboresha mbio au nguvu.
| Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Magnesi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |