Maelezo ya Kihistoria ya falme tatu: Kongo, Matamba, na Angola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maelezo ya Kihistoria ya Falme Tatu: Kongo, Matamba na Angola (kwa Kiitalia: Istorica Descrizione de' tre regni Congo, Matamba ed Angola) ni kitabu kirefu kilichoandikwa na Giovanni Antonio Cavazzi da Montecuccolo, mmisionari wa shirika la Kikatoliki la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Italia. Alitumwa kama mmisionari nchini Angola alipofanya kazi kati ya miaka 1654 na 1677.

Kazi hiyo iliagizwa na Ofisi kwa Uinjilishaji wa Mataifa katika Vatikani, wakati Cavazzi aliporudi kutoka safari yake ya kwanza ya umisionari kwenda Angola mnamo 1668. Alikamilisha rasimu ya maandishi hayo karibu 1671, lakini alipata upinzani kutoka kwa Kanisa, haswa kwa sababu ya hadithi nyingi za miujiza, ambazo zilizuia kuchapishwa kwake. Baada ya muda, kazi ya kuhariri kazi hiyo alipewa mwingine, Fortunato da Alamandini, ambaye alikihariri, na mwishowe kilichapishwa mnamo 1687 huko Bologna. Toleo la pili lilionekana huko Milano mnamo 1690.

Cavazzi alianza kuandika kazi hii karibu na mwaka 1660, labda baada ya kushuhudia kuongoka na kubatizwa kwa Malkia Njinga, ambako aliona kama miujiza.[1] Aliandika rasimu kadhaa za kazi ambayo aliiita "Misione Evangelica" ambayo aliikamilisha mnamo 1668[2].

Muswada wake uko katika milki ya familia ya Araldi ya Modena, Italia, ulitafsiriwa kwa Kiingereza na kutolewa kwenye ukurasa wa tovuti wa John Thornton, pamoja na utangulizi kamili[3].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Tafsiri[hariri | hariri chanzo]

  • Labat, Jean-Baptiste (1732). Relation historique de l'Ethiopie occidental. Paris: Delespine. 5 vols.
  • Saccardo, Graziano [da Luggazano] (1965) ed. and trans. Descrição histórica dos três reinos Congo, Angola e Matamba. Lisbon: Agência Geral do Ultramar. 2 vols.

Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo]

  • Cuvelier, Jean (1949). "Notes sur Cavazzi," Zaire 3: 175-84.
  • Pistoni, Giuseppe (1969)"I manoscritti 'Araldi' di Padre Giovanni Antonio Cavazzi da Montecuccolo," Atti e memorie, Accademia di scienze, lettere e arti di Mondena 2: 152-65.
  • idem (1972). Fra Giovanni Antonio Cavazzi da Montecuccolo: Documenti inediti Modena
  • Thornton, John (1979). "New Light on Cavazzi's Seventeenth Century Description of Kongo," History in Africa 6: 253-64.