Wakapuchini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakapuchini ni watawa Wafransisko wa Kanisa Katoliki.

Idadi yao inapita ndugu wanaume 10,000 duniani kote wakiongozwa na ndugu Mauro Jöhri wa kanda ya Uswisi.

Jina linatokana na neno la Kiitalia "cappuccio", lenye maana ya kikofia kilichoshonwa kwenye kanzu yao ya rangi ya kahawia.

Tawi hilo lilianzishwa na Mathayo wa Bascio pamoja na Ludoviko wa Fossombrone na Rafaeli wa Fossombrone, ambao walilenga maisha ya kifukara kuliko yaliyofuatwa na Ndugu Wadogo wenzao.

Urekebisho huo, uliojitahidi sana kufuata kikamilifu kanuni ya Ndugu Wadogo na mifano ya mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, ulipata kibali cha Papa Klementi VII mwaka 1528.

Baada ya hapo shirika likaenea na kuzaa matunda mengi ya utakatifu kuanzia bradha Felix wa Cantalice hadi Pio wa Pietrelcina.


[hariri] Viungo vya nje