Lordi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lordi
Lordi, 2023
Lordi, 2023
Maelezo ya awali
Asili yake Helsinki, Finland
Aina ya muziki Hard rock / heavy metal,power metal, shock rock, horror rock
Miaka ya kazi 1991 – mpaka sasa
Studio Sony BMG, GUN, The End, Drakkar Records
Ame/Wameshirikiana na Dolchamar, Punaiset Messiaat, Arthemesia, Deathlike Silence, Wanda Whips Wall Street, Double Beat Und Bodys
Tovuti www.lordi.fi
Wanachama wa sasa
Mr. Lordi
Amen
Hiisi
Mana
Hella
Wanachama wa zamani
G-Stealer
Magnum
Kalma
Enary
Kita
Otus
Awa
OX

Lordi ni bendi ya muziki wa hard rock/heavy metal kutoka mjini Helsinki, Finland. Wazo la kubuni jina la Lordi lilitolewa mnamo mwaka wa 1992, ingawa bendi ilikuwa haijaanzishwa hadi ilipokuja kuanzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1996 na Tomi Putaansuu (maarufu kama "Mr. Lordi")[1] wa Rovaniemi, Finland.

Wanachama wa Lordi wanaeleweka kwa jinsi wanavyojieleza kwa mavazi ya mijitu ya kutisha wakati wanapofanya maonyesho yao au hata video zao. Hivyo Lordi hujulikana pia kwa jina la "The Finnish Monsters" na "The Monsters of Finland".

Siku za mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Putaansuu alikuwa akicheza katika bendi ndogo ya mjini Rovaniemi. Aliondoka bendini kwa kufuatia wanachama wengine wa katika bendi hawakubaliana na uanzishaji wa muziki wakiwa ukumbini hasa kwa kuingiliana na vipengele vya staili ya bendi ya KISS. Putaansuu akaanza kutengeneza muziki wa demo chini ya jina la Lordi kunako mwaka wa 1991 na kuendelea kufanya hivyo kwa miaka kadhaa ya usoni. Mnamo mwaka wa 1995 ametengeneza wimbo wa "Inferno" na muziki wa video kwa ajili mradi fulani wa shule. Video haikutolewa kwa kufuatia Putaansuu hakuvaa kinyago kwenye video hiyo ndiyo sababu iliyopelekea video isitolewe.

Baada ya "Inferno", Putaansuu akaota. Katika ndoto hiyo, ilimwonyesha yeye akiwa akiwa kwenye onyesho na kuna kiunzi cha mifupa kinacheza juu ya jukwaa. Alipoamka, akaelewa kwamba Lordi inapaswa kuwa bendi ya muziki wa Heavy metal iliojawa na vizuka. Lile jitu la kutisha alioiona kwenye ndoto hatimaye akaja kuwa mpiga gita wao Kalma.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Studio Albamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Albamu Nafasi Iliyoshika
UK UK Rock FIN GER AUT BEL DEN EST FRA GRE NOR POL SWE SWI EU US Ind US Heat
2002 Get Heavy - - 3 - - - - - - - - - - - - - -
2004 The Monsterican Dream - - 4 70 - - - - - - - - - - - - -
2006 The Arockalypse 100 - 1 7 11 13 16 4 98 1 21 29 1 8 8 - -
2008 Deadache - 38 5 33 51 - - - - - 39 35 42 73 71 37 13
2010 Babez For Breakfast
  • Albamu 5
  • Imetolewa: 15 Septemba 2010
  • Studio: Sony BMG
- - 9 66 71 - - - 113 26 - - - - - - -
2013 To Beast or Not To Beast - - - - - - - - - - - - - - - - -
2014 Scare Force One
2016 Monstereophonic – Theaterror vs. Demonarchy
2018 Sexorcism
2020 Killection
2021 Lordiversity

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Finns dismayed after Eurovision monsters unmasked", Reuters, 26 Mei 2006

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu muziki wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lordi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.