Nenda kwa yaliyomo

Lee van Cleef

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lee Van Cleef, 1952.

Lee Van Cleef (Alizaliwa tar. 9 Januari 192516 Desemba 1989). Alikuwa muigizaji wa filamu wa marekani, aliyeonekana zaidi katika filamu za western hasa filamu za mapigano.

Umbo lake la uso ambamo macho yamezama ndani yamemfanya kiupeo kuwa yeye ni "mtu mbaya" ingawaje mara nyingi alikuwa akicheza kama shujaa, Mwindaji wa kimaslahi katika filamu ya For a Few Dollars More.

Masiha ya Mwanzo

[hariri | hariri chanzo]

Van Cleef alizaliwa mjini Somerville, New Jersey na mzee Clarence Leroy Van Cleef, Sr mama yake Marion Lavinia Van Fleet, Familia nzima ilikuwa ina asili ya Kiholanzi, ya Kisweden, ya Kibelgiji na ya Kiingereza.

Cleef pia alifanya kazi katika jeshi la marekani (Navy) katika kipindi cha vita ya pili ya dunia kisha baadae akafanya shughuli za kihasibu kidogo sio sana siku kadha mbeleni akawa muigizaji.

Mwanzoni aligiza katika filamu fulani hivi ya Broadway, Kampuni ilyokuwa inachapisha vitabu vya hadithi mbali mbali, Na humo hakuwa nafahamika sana kwasababu wadhfa ulikuwa mdodogo.

Filamu yake ya kwanza kucheza kama mtu wa hali ya juu ilikuwa moja kati ya filamu za western ilyokuwa inaitwa High Noon aliocheza na Gary Cooper, Japokuwa katika filamu alicheza kama kibara bado heshima yake ilikuwa kubwa. Pia alipata kuonekana kidogo katika filamu ya Beast from 20,000 Fathoms, Kama mpigaji bunduki kwa haraka zaidi.

Mnamo mwaka 1956 alicheza kama nyota mshiriki akiwa na Peter Graves katika filamu za B-grade filamu za kisayansi filamu iliitwa It Conquered the World.

Maisha Binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Lee Van Cleef alifariki dunia kwa ugonjwa wa moyo (heart attack) mjini Oxnard, California na kuzikwa katika makabuli ya Forest Lawn - Hollywood Hills Cemetery yaliyopo mjini Los Angeles, Sehemu hiyo ni yakuzikia watu maarufu tu hasa waigizaji wa filamu. Lee van Cleef alifariki dunia tar. 16 Desemba 1989.

Cleef pia amepoteza ncha yake ya kidole cha kati cha mkono wa kulia wakati anajenga chumba cha kuchezea binti yake. Kidole kinaweza kuonekana katika filamu ya The Good, the Bad, and the Ugly kakifunga katika mkono, wakati wa mapigano ya bastola na katika sini zake za mwanzo, Moja kati ya sini ya mwanzo ni The Grand Duel.

Filamu Alizocheza

[hariri | hariri chanzo]
Lee Van Cleef katika moja kati ya filamu za Western.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]