Nenda kwa yaliyomo

Lameck Ditto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lameck Ditto
Jina la kuzaliwa Dotto Bernad Bwakeya
Pia anajulikana kama "Lameck Ditto"
Amezaliwa 8 Januari 1987 (1987-01-08) (umri 37)
Asili yake Kagera/Morogoro, Tanzania
Aina ya muziki Zouk
Soul
Kazi yake Mwimbaji
Mwanamuziki
Mtunzi wa nyimbo
Mtayarishaji
Ala Ngoma
Sauti
Miaka ya kazi 2000 - hadi leo
Ame/Wameshirikiana na Afande Sele<r>Mrisho Mpoto
Watupori
Tovuti [1]


Dotto Bernad Bwakeya (a.k.a Lameck Ditto [2] Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2013 kwenye Wayback Machine.) ni mwimbaji wa muziki wa Bongo Flava aliyeibuliwa na rapa mkongwe Afande Sele mwaka 2003 katika tamasha la kuibua vijana wadogo wenye vipaji lilioandaliwa na kituo cha Redio Ukweli kilichokuwa na makao yake Morogoro nchini Tanzania.

Kipindi hicho akiitwa Dogo Ditto alishirikishwa kwenye nyimbo zote za albamu ya pili ya Afande Sele Darubini Kali ukiwemo wimbo huo wa Darubini Kali [3] pia baadae mwaka 2004 Lameck Ditto alimshirikisha Afande Sele katika wimbo wake wa kwanza kurekodi kama msanii anayejitegemea wa Dunia inamambo uliofanikiwa kukamata chati katika ukanda wa Afrika Mashariki [4] Lameck Ditto au Dogo ditto kwa kipindi hicho mwaka 2005 alishiriki kuasisi kundi la Watupori akiwa na Afande Sele na Mc Koba baada ya kundi la Ghetto Boys kuvunjika.

Watupori, kundi lilokuwa na maskani yake mkoani Morogoro, walifanikiwa kutoa nyimbo kama Usinichukie, Nafsi ya mtu na Sana Tu [[5]] ambazo zilitamba na kukamata chati za juu. Watupori haikudumu sana baada ya mikwaruzano ya hapa na pale ambayo inasemekana ilichangiwa na Ditto kutakiwa Bongo Record ya P Funk ambaYe alikuwa tayari kumpatia mkataba wa kurekodi albamu ya peke yake nje ya Watupori [6] Ilihifadhiwa 10 Septemba 2017 kwenye Wayback Machine..

Lameck Ditto akifuatana na Mc Koba waliachana na Afande Sele na kuungana wakarekodi albamu yao ya kwanza katika Studio za Bongo records walifanikiwa kutoa wimbo mmoja tu wa Ulibisha Hodi ambao nao ulifanya vyema kabla ya wote kujiunga katika kundi la La familia lililokuwa likiongozwa na Chid Benz ambalo pia liliundwa na Kassim Mganga, Tunda Man, O Ten, Chiku Ketto na Mc Koba hapo ndipo Rasmi akaanza kutumia jina la Lameck Ditto. Akiwa LAfamilia alishirikishwa katika nyimbo kama Ngoma Itambae (Dar es Salaam Stand Up na Muda Umefika ft Chiku Keto [7].

mwaka 2008 Ditto akajiunga na Taasisi ya kukuza na kulea vijana wenye vipaji ya Tanzania House Of Talent THT ili kujiongezea ujuzi katika fani hii ambapo alifanikiwa kutoa nyimbo kama Wapo, Tushukuru kwa yote na Niamini.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lameck Ditto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.