Afande Sele

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Afande Sele

Seleman Msindi au Afande Sele (amezaliwa tar. 24 Aprili 1976) ni msanii wa muziki wa hip hop na Bongo Flava kutoka Mkoani Morogoro, Tanzania. Amewahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards mnamo mwaka 2004 kutokana na nyimbo yake ya 'Mtazamo' ambayo aliimba na Solo Thang na Professor Jay.pia alishinda tuzo ya (mkali wa rymes) mwaka [2003] kutokana na nyimbo yake ya 'darubini kali' aliyosmshirikisha Dogo Ditto.Ni muasisi wa makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori' ,yaliozaliwa na kufia mjini Morogoro kwa kufuatana na alikuwa msanii wa kwanza kuujaza uwanja wa mpira wa miguu wa JAMUHURI mjini morogoro alipozindua albam yake ya kwanza ya 'MKUKI MOYONI'.Aliongoza kampeni ya maleria mwanzoni mwamiaka ya 2005 na 2007..Mwanzoni wa mwezi wa 11 mwaka 2012 alitangaza rasmi kufanya kazi kama kundi jipya la watu pori baada ya kufanya kazi na MC KOBA ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda kundi la watu pori miaka ya nyuma.

Maisha Binafsi[hariri]

Afande Sele ana mke na watoto wawili wa kike,Tunda na Sanaa wanaishi pamoja na mkewe huko mkoani Morogoro.


Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Afande Sele kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.