Nenda kwa yaliyomo

Kujenga mwili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mazoezi ya Kujenga mwili

Kujenga mwili ni mazoezi yanayofanywa ili kudhibiti na kukuza misuli. Wanaojenga misuli si tu mazoezi wanayofanya bali pia hutumia lishe maalum ili kuipa miili yao aina za chakula, na madini yanayohitajika. Kujenga mwili ni mchakato mgumu unaochukua muda na huhitaji nidhamu ya hali ya juu ili kuufanikisha, hivyo umewashinda wengi.

Watu hujenga miili kwa sababu tofauti: sababu za kikazi kwa wale ambao hufanya kazi zinazohitaji nguvu ya kimwili kama wanajeshi, kutumia wakati wa ziada, na pia kushiriki mashindano ya kujenga mwili. Wanaoshiriki mashindano ya kujenga mwili hushikilia mazoezi ya kujenga misuli kwa kina na wana nidhamu ya hali ya juu. Mashindano hayo hufanywa kati ya nchi tofauti, bara na hata ya dunia nzima. Mashindano kama ya "International Federation of Body Builders -IFBB ya tuzo la Mr. Olimpia", na "National Armature Body-Builders Association NABBA ya tuzo la Universe Championships" ni mojawapo ya mashindano ya kujenga misuli yanayojulikana dunia mzima.

Historia ya Kujenga mwili

Zoezi la kuinua mawe ili kujenga misuli lilifanyika zama za kale nchini Misri, Ugiriki na Tamilakam.[1] Upande wa magharibi katika nchi za Ulaya zoezi hili lilinawiri kati ya mwaka wa 1800 na 1953 wakati wanaume wa miraba walionyesha ubingwa wao na kushindana hadharani. Hata hivyo, wakati ule washindi hawakushindina ujenzi wa misuli bali walishindana ukubwa kwani hata wenye kitambi walishiriki. [2]

Hivi leo mashindano ya kujenga misuli yamekomaa yakishirikisha si tu wanaume bali pia wanawake. Mwaka wa 2000 mashirika husika ya kujenga misuli yalijaribu kupiga hatua kushirikisha mchezo huu Olimpiki lakini hawakufaulu.

Taratibu za Kujenga mwili

Wataalamu, mashirika tofautitofauti na jimu wana taratibu tofautitofauti za kujenga misuli. Hata hivyo taratibu hizi hutofautiana kidogo. Mambo muhimu ya kufuatilia ni:

  • mazoezi ya kuinua chuma
  • chakula chenye wingi wa kalori
  • utumizi wa virutubisho (kama Keretini na Protini ya Whey)
  • ulaji wa protini
  • kupumzisha mwili vizuri baada ya zoezi
  • Kutoshiriki mazoezi ya Cardio

Tanbihi

  1. Karthikeyan, D. (Januari 12, 2013). "Locked horns and a flurry of feathers" – kutoka www.thehindu.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Schwarzenegger, A. (1999). The New Encyclopedia of Bodybuilding. Fireside, NY: Simon & Schuster. ISBN 0684857219.

Viongo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kujenga mwili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.