Hippo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Annaba (zamani: Hippo Regius, Kar.:عنابة anaba, Kifar. Bône) ni mji katika Algeria kwenye mwambao wa Mediteranea mwenye wakazi 385,000 (2005). Kuna chuo kikuu chenye wanafunzi 40,000.

Mji ulianzishwa kwa jina la Hippo kama koloni ya Wafinisia katika karne za KK. Tangu 46 KK ilikuwa sehemu ya Dola la Roma.

Mkazi wake mashuhuri alikuwa Agostino Aurelio aliyejulikana kama Agostino wa Hippo aliyekuwa askofu wa mji tangu 396 BK. Agostino aliandika hapa sehemu kubwa ya vitabu vyake. Aliaga dunia wakati wa uvamizi wa Wavandali waliofanya Hippo kuwa mji mkuu wa ufalme wao.

Tangu mwaka 698 Hippo ilitekwa na Waarabu Waislamu waliouharibu wakaunda mji mpya kando la maghofu ulioitwa "Beleb-El-Anab". Jina hili likaendelea kubadilika kuwa "Annaba" wa mji wa leo.