Nenda kwa yaliyomo

Christopher Richard Mwashinga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Christopher Richard Mwashinga

Christopher R. Mwashinga, Jr (amezaliwa Januari 9, 1965) ni mchungaji, mwanateolojia, mwandishi wa vitabu na mshairi kutoka nchi ya Tanzania anayeishi nchini Marekani. Amechapisha vitabu vya mashairi, teolojia, utume na historia ya dini. Mashairi yake yamechapishwa Singapore [1], Tanzania [2], Kenya [3] na Marekani[4]. Anaandika vitabu kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Asili na Familia

Alizaliwa akiwa mtoto wa tatu wa mzee Richard Male Mwashinga kutoka katika ukoo wa kichifu (Mwene) katika kitongoji cha Igawilo, jijini Mbeya, na mama Christine Mwaselela toka kitongoji cha Inyala, Mbeya, nchini Tanzania. Kwa miaka mingi wazazi wake waliishi katika eneo la Uyole ndani ya Jiji la Mbeya.[5]

Elimu

Christopher R. Mwashinga alisoma katika shule ya msingi Ngare-Nairobi, mkoani Kilimanjaro. Alihitimu elimu ya sekondari katika shule za Igawilo Sekondari iliyoko jijini Mbeya 1988 kidato cha nne na Shule ya Sekondari ya Wavulana Songea 1991kidato cha sita. Alipomaliza masomo ya sekondari, alijiunga na Chuo Kikuu Kigezo:Arusha kusomea theolojia mwaka 1993. Mwaka 1994 alihamia Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki,Baraton nchini Kenya alipotunukiwa shahada ya kwanza BA katika theolojia mwaka 1997[6]. Vile vile alitunukiwa shahada mbili za uzamili katika mambo ya theolojia,Master of Divinity MDiv (2008)[7] na Master of Arts, MA in Systematic Theology,(2010)[8],zote katika Chuo Kikuu cha Andrews kilichopo katika jimbo la Michigan nchini Marekeni; mahali ambapo baadaye alijiunga na masomo ya shahada ya juu ya Udaktari wa Falsafa (Ph.D) katika fani ya theolojia.[9]

Huduma kwa Vijana na Wanafunzi

Christopher Richard Mwashinga

Alifanya kazi kama Mkurugenzi wa idara ya Elimu na Vijana katika Jimbo la Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato kuanzia 1997-2005.[10][11] Jimbo la Mashariki mwa Tanzania linajumuisha mikoa ya Dar Es Salaam, Morogoro, Dodoma, Pwani, Mtwara na Lindi kwa upande wa Tanzania bara, na mikoa yote ya Tanzania visiwani. Kazi yake ilimpatia fursa ya kukutana na wakuu wa vyuo vikuu vingi katika mabara matano duniani. Sauti yake ilikuwa ikisikika mara kwa mara katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki hasa kati ya 1992-2005. Kila mwaka alikuwa akifanya mikutano mikubwa ya Injili katika majumba ya mikutano ya vyuo vikuu mbalimbali kama vile Nkrumah Hall (Chuo Kikuu cha Dar es salaam), Multi-Purpose Hall (Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine), New Assembly Hall (Chuo Kikuu Mzumbe); na katika taasisi nyingine nyingi za elimu ya juu nchini Tanzania kama vile Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba, Muhimbili, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Chuo cha Ufundi Arusha, Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam, Chuo Kikuu Arusha, Chuo cha Ufundi Mbeya n.k.[12][13] Vile vile katika mikutano ya kila mwaka ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki alikuwa mhutubu katika vyuo vikuu mbalimbali kama vile Chuo Kikuu cha Nairobi,Chuo Kikuu cha Moi, Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Baraton, na Chuo cha Teknolojia cha Mombasa, vilivyopo nchini Kenya. Katika nchi ya Uganda alihutubu katika Chuo Kikuu cha Makerere na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbarara. Mikutano yake ilihudhuriwa na wanafunzi na wahadhiri wengi katika vyuo hivyo. Katika hotuba zake pamoja na kuhubiri Injili, alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanafunzi na jumuiya za vyuo vikuu kutokata tamaa na kuweka malengo ya juu katika kutoa mchango wao wa huduma bora kwa jamii kwa ujumla. Mara nyingi alikemea ubaguzi, ubinafsi, kupenda pesa zaidi kuliko kupenda watu, na alisisitiza kwamba ili nchi yoyote iendelee, wasomi wake lazima wawajibike katika kufanya kazi kwa bidii na maarifa,huku wakiwajali wananchi wa kawaida ambao wengi wao hawajapata fursa yakusoma katika taasisi za elimu ya juu kama wao. Alizoea kuwakumbusha wasikilizaji wake kwamba maendeleo siku zote yanaanzia chini kwenda juu na siyo kinyume chake. "Wananchi wa kawaida wakiendelea, nchi itaendelea." Siku zote aliwasisitizia juu ya umuhimu wa kuwa wazalendo kweli kweli na kwamba ni muhimu kuwa na mapenzi mema na nchi yao. Aliwakumbusha wasomi kwamba Ukristo wa kweli na uzalendo wa kweli havipingani. Mtu anaweza kuwa Mkristo wa kweli na mzalendo wa kweli kwa wakati mmoja. Vile vile mtu anaweza kuwa na mafanikio kitaaluma na akawa na bidii katika maswala ya imani. Kitabu chake kiitwacho Rays of Hope: Living to Make a Difference ni makusanyo ya baadhi ya hotuba zake zilizopendwa sana na jumuiya za vyuo vikuu vya Tanzania. Vile vile baadhi mahuburi yake aliyoyahubiri katika vyuo vikuu vingi yamechapishwa katika kitabu kinachoitwa: Enduring the Cross: Messages of Salvation and Hope.[14]

Ushairi na Uandishi

Ushairi

Kwa zaidi ya miaka thelathini, Christopher Mwashinga amekuwa akiandika mashairi ya Kiswahili na Kiingereza. Mashairi yake ya Kiingereza yamechapwa katika magazeti na vitabu maarufu kakika nchi mbalimbali duniani. Nchini Tanzania mashairi yake ya Kiingereza yalitokea zaidi katika gazeti la Sunday News hasa katika miaka ya tisini.[15] Yalichapishwa vile vile katika nchini Kenya katika gazeti maarufu la "Sunday Nation" [16]. Yalichapishwa pia nchini Singapore, na Marekani. Nchini Marekani, mashairi yake yalichapishwa na makampuni makubwa kama vile The League of American Poets[17] na Famous Poets Press katika kitabu chao cha Mashairi Makuu ya Ulimwengu wa Magharibi (Great Poems of the Western World)[18]; [19]. Mashairi yake ya Kiswahili yamechapishwa katika magazeti na majarida mbalimbali pia ikiwa ni pamoja na gazeti la Sauti Kuu[20] Mashairi yake mengi yanapatikana katika vitabu vyake vitano vya Kiingereza, ''Beaches of Golden Sand'': Inspirational Poems; Windows of Love; Ocean of Grace; Short Poems of Christopher Mwashinga na Collected Poems of Christopher Mwashinga. Mashairi yake ya Kiswahili yamechapishwa katika vitabu zaidi ya kumi ikiwa ni pamoja na Sauti Toka Ughaibuni; Kilele cha Tumaini; Tumaini Lenye Baraka: Diwani ya Christopher Mwashinga; Sauti ya Faraja na Matumaini; Mdomo Mmoja na Masikio Mawili: Mashairi ya Watoto ;Mionzi ya Matumaini; Njia ya Matumaini; "Kazi za Christopher Mwashinga, Juzuu ya 3: Mashairi na Mwenge wa Matumaini. Mashairi yake pia yamekuwa yakighanwa au kusomwa katika vyombo mbalimbali vya habari kama vile televisheni na redio katika nchi mbalimbali duniani.[21] ; [22] ;[23]; [24] Historia ya kazi yake ya kutunga mashairi ya Kiswahili inapatikana hapa Ushairi wa Christopher Richard Mwashinga.

Uandishi wa vitabu vingine

Pamoja na vitabu vya mashairi, ameandika vitabu vingine zaidi ya ishirini ikiwa ni pamoja na: A History of Christianity in East Africa: The Beginning and Development of Missions ; Rays of Hope: Living to Make a Difference, Enduring the Cross: Messages of Salvation and Hope, Barua na Mashairi , Mission Theology and a History of Christian Missions in East Africa Utume na Ukristo Katika Afrika Mashariki, Uadventista Barani Afrika: Channgamoto na Fursa za Ukuaji, pamoja na majuzuu kadhaa ya makusanyo ya kazi zake za Kiingereza na za Kiswahili ikiwa ni pamoja na The Works of Christopher Mwashinga Vols I, II, III. IV. Pia Kazi zake za Kiswahili Juzuu ya 1,2,3,na 4. Journals and Diaries (1) Berrien Springs, MI: Maximum Hope, 2017</ref>. Vitabu vyake vimechapishwa na makala zake za kisomi na kitaaluma zimechapishwa na makampuni mbalimbali ya uchapishaji ikiwa ni pamoja na AuthorHouse, Journal of the Adventist Theological Society; Journal of Adventist Mission Studies; Andrews University Seminary Student Journal na vingine vimechapishwa na Maximum Hope Books (Independent-publishing) kwa kushirikiana na Amazon.com.

Uanachama katika vyama vya kitaaluma

  • Adventist Theological Society
  • American Academy of Religion
  • Michigan Academy of Science, Arts, and Letters
  • American Academy of Poets
  • Evangelical Theological Society

Machapisho yake

Vitabu vya Kiswahili

Ushairi

Vitabu vingine

Mradi wa makusanyo ya kazi za Kiswahili za Christopher Mwashinga

Vitabu vya Kiingereza

Mradi wa makusanyo ya kazi za Kiingereza za Christopher Mwashinga

Tanbihi

  1. El Shadai Magazine.
  2. Tanzania's Sunday News of October 1991; January 1992;
  3. Kenya's Sunday Nation of 18 June 1995; 13 August 1995
  4. The League of American Poets' Anthology: A Treasury of American Poetry Vol. III, published in 2007; Literature Evangelist Magazine published by the General Conference of Seventh-day Adventists, June 1996; and Great Poems of the Western World, 2010
  5. Moments of my Christian Experience, Berrien Springs, MI: Maximum Hope, 2016
  6. Gazeti la Parapanda Gazeti Na. 2, Toleo la 1, Januari-Juni, 2004
  7. IN TOUCH Volume 2 Issue 3. A Newsletter of the Seminary Student Forum, March 2008. Andrews University.
  8. Bruce Bauer, ed. Diversity: Challenges and Opportunities. Berrien Springs, MI: Department of World Mission, Andrews University, 2010, 79-82.
  9. The Andrews University Seminary Student Journal Vol. 2, No. 1, 2016: 33-51
  10. Mwashinga, Enduring the Cross: Messages of Salvation and Hope, 250-252
  11. Seventh-day Adventist Year Book 2005, p. 51
  12. Christopher Mwashinga,Jr The Works of Christopher Mwashinga Volume II: Sermons, Speeches, and Poems (Berrien Springs, MI: Maximum Hope Books,2014),609.
  13. Seventh-day Adventist Year Book 2005, p. 51
  14. Enduring the Cross: Messages of Salvation and Hope, 250-252
  15. Tanzania's Sunday News of October 6, 1991; Sunday News January 19,1992; Sunday News May 10, 1992
  16. Kenya's Sunday Nation of June 18, 1995; Jaly 9, 1995; November 26, 1995
  17. The League of American Poets' Anthology: A Treasury of American Poetry Vol. III, published in 2007
  18. Great Poems of the Western World, 2010
  19. PS:It's Poetry: An Anthology of Eclectic Contemporary Poems Written by Poets Around the Globe.
  20. Sauti Kuu Alhamisi, Januari 30, 2020; Alhamisi, Februari 13,2020; Alhamisi, Januari 13-19, 2022.
  21. https://www.youtube.com/watch?v=4lCJjpEFs3Q
  22. https://www.youtube.com/watch?v=EkCL5NfJFxQ
  23. https://www.youtube.com/watch?v=y3WXarWW5SQ
  24. https://www.youtube.com/watch?v=yvcEfEt7BH4