Bunilizi ya kinjozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Bunilizi ya kinjozi (au bunilizi ya kifantasia) ni utanzu fulani wa fasihi andishi. Katika bunilizi hiyo mwandishi anatumia matukio au wahusika wasio wa kawaida. Mifano ya bunilizi ya kinjozi katika fasihi ya Kiingereza ni "A Midsummer Night's Dream" (Ndoto ya Usiku Mmoja) ya William Shakespeare, "Gulliver's Travels" (Safari za Guliveri) ya Jonathan Swift, au "The Lord of the Rings" (Bwana wa Mapete) ya J.R.R. Tolkien.

Bunilizi ya kinjozi hutofautishwa na bunilizi ya kisayansi kwa vile haisifu mambo ya teknolojia bali inatumia maajabu na viumbe vya visasili.

[hariri] Marejeo

Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine