Fasihi andishi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fasihi andishi ni sanaa itumiayo maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
Fasihi andishi hugawanyika katika matawi mawili: nathari na ushairi.
Pia fasihi andishi ina tanzu nyingi mbalimbali, hasa riwaya, tamthiliya, insha, shairi n.k.
Kulingana na mada ya kazi ya kifasihi, inawezekana kutofautisha bunilizi na kazi zinazowakilisha ukweli.
Marejeo [hariri]
Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.