Majadiliano:Bunilizi ya kinjozi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bunilizi ya kinjozi? Au Bunilizi la Kinjozi? Haya, pia sijawahi kusikia Kiswahili hiki - na wala hakuna kwenye kamusi za Kiswahili. Sijui imekuwaje. Labda tuseme "UBUNIFU WA KINJOZI" - lakini kwa hili? Tena, sijui niite vipi tafsiri ya science fiction. Hapa nimeona wakiandika "bunilizi la kisayansi". Kwenye Alien vs. Predator, nimeandika "uzushi wa kisayansi". Tutumie ipi kati ya hizo?--MwanaharakatiLonga 08:22, 24 Aprili 2010 (UTC) [jibu]

Nilivyotaja kwenye marejeo, mambo hayo yametoka Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia iliyoandikwa na Profesa Wamitila, maana yake ndivyo ilivyofundishwa chuoni. Naona tuendelee na bunilizi (kwa Kiingereza ni 'fiction'). Tena, wanaandika "bunilizi ya ...", k.m. bunilizi ya kisayansi 'science fiction', bunilizi ya kitawasifu 'autobiographical fiction', bunilizi ya kiutendi 'epic fiction' n.k. Haya, Kiswahili kimepanuka, hasa istilahi za elimu ya juu. Tusijitenge na wataalamu. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:41, 24 Aprili 2010 (UTC)[jibu]
Haya, basi nitafuata hao wataalamu. Wako,--MwanaharakatiLonga 12:22, 24 Aprili 2010 (UTC)[jibu]