Asuncion
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Jiji la Asunción | |
| Nchi | Paraguay |
|---|---|
Asunción ni mji mkuu wa Paraguay. Jiji lina wakazi milioni 1.6. Jina kamili kwa Kihispania ni "Nuestra Señora Santa María de la Asunción" (Mama yetu Mtakatifu Mariamu wa kupaa). Maana ya "asuncion" ni "kupaa mbinguni" kwa kukumbuka siku ya kuundwa kwa mji na conquistador Juan de Salazar tarehe 15 Agosti 1537 ambayo ni sikukuu ya kupaa kwake Mariamu mbinguni katika desturi ya kikatoliki.
Jiji ni kitovu cha kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa ya nchi.
Asuncion iko kando la mto Paraguay ikitazama mdomo wa Río Pilcomayo upande wa Argentina.
Ni kati ya miji ya kwanza iliyoundwa na Wahispania katika Amerika Kusini. Kwa sababu hiyo huitwa mara nyingi "Mama wa miji".
| Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Asuncion kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |