Nenda kwa yaliyomo

Anna Tibaijuka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Anna Kajumulo Tibaijuka)
Profesa Anna Tibaijuka Mbunge


Muda wa Utawala
28 Novemba 2010 – 23 Disemba 2014
Rais Jakaya Kikwete
mtangulizi John Zefania Chiligati

Mkurugenzi Mtendaji wa UN–HABITAT
Muda wa Utawala
Machi 2006 – 2010
aliyemfuata Joan Clos i Matheu

Mbunge
kwa Muleba Kusini
Muda wa Utawala
Novemba 2010 – November 2020
mtangulizi Wilson Masilingi
aliyemfuata Oscar Ishengoma Kikoyo
Majority Unopposed

tarehe ya kuzaliwa 12 Oktoba 1950 (1950-10-12) (umri 74)
Kagabiro, Muleba, Tanganyika
utaifa Mtanzania
chama CCM
watoto 4
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kilimo, Uppsala, Uswidi
Awards Gothenburg Award
tovuti annatibaijuka.org

Anna Kajumulo Tibaijuka (alizaliwa 12 Oktoba, 1950) ni mtaalamu wa Uchumi wa kilimo, pia mwanasiasa wa Tanzania katika CCM na alikuwa Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini tangu mwaka 2010 hadi 2020.

Aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. [1]

Familia na masomo

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Kagabiro karibu na Muleba, Tanzania katika familia ya wakulima wadogo.

Miaka 1958-1961 alisoma shule ya msingi Kaigara akaendelea kwenye shule ya kati ya Wasichana ya Kashozi – Kamukukubwa halafu shule ya sekondari ya wasichana Rugambwa, Bukoba, 1966 – 1969. Kutoka hapo alipokewa Form V ya Marian Girls, Morogoro.

Baada ya huduma kwenye Jeshi la Kujenga Taifa akajiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Kilimo, Morogoro 1972 - 1975 hadi digrii ya kwanza. Akaajiriwa kama Mhadhiri Mzaidizi kwenye Idara ya Uchumi. Mwaka huohuo akafunga ndoa na Wilson Kamuhabwa Tibaijuka, aliyekuwa kwa wakati huo afisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Uswidi.[2] Alizaa naye watoto wanne, Muganyizi (1976), Kemilembe (1979), Kagemulo (1986) na Kankiza (1991). Wakati wa kukaa Uswidi alisoma hadi digrii ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo, Uppsala.

Mwaka 1979 familia ilirudi Tanzania na Anna Tibaijuka alianza kufundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitengo cha Utafiti wa Uchumi. 1981 alifadhiliwa kurudi Uswidi na kufuata kozi ya PhD aliyomaliza 1983. Akarudi Dar es Salaam akafundisha tena uchumi.

Mwaka 1998 aliteuliwa kujiunga na ofisi kuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) mjini Geneva alikoongoza idara ya nchi maskini. Baada ya miaka miwili huko Geneva aliombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kuongoza Kituo cha Makazi Duniani (UN-Habitat Centre). Alifanya mabadiliko na matengenezo katika kazi ya kituo hii hadi Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kupandisha hadhi ya kituo kuwa "United Nations Human Settlements Programme" (UN-HABITAT) yenye makao makuu huko Nairobi. Tibaijuka alichaguliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa kitengo hiki kipya mwaka 2002 akapewa cheo cha Katibu Mkuu Msaidizi na hapo alikuwa mwanamke Mwafrika wa kwanza aliyefika ngazi hii katika historia ya UM hadi leo (2017).

Mwanasiasa wa Tanzania

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2010 alirudi Tanzania baada ya kumaliza kipindi chake cha pili cha kuongoza UN-HABITAT. Alishiriki katika uchaguzi mkuu akachaguliwa mbunge wa Muleba Kusini kwa niaba ya CCM.

Baada ya uchaguzi aliingia katika serikali ya Mizengo Pinda akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mwezi wa Desemba 2014 rais Jakaya Kikwete alimwachisha Tibaijuka kutoka wizara yake kwa sababu aliwahi kupokea pesa kutoka James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing (VIPEM) aliyehusika katika kashfa ya rushwa ya Tegeta escrow. [3]. Alikosolewa kwa kupokea milioni 1 ya USD kwenye akaunti yake ya binafsi.

Tibaijuka alijaribu kujitetea kuwa pesa ilikuwa msaada kwa ajili ya taasisi ya Joha Trust inayogharimia shule ya wasichana ya Barbro Johansson na ya kwamba pesa ilipitia tu katika akaunti yake ya binafsi.[4]

Mwaka 2015 alipendelewa tema kugombea ubunge wa Muleba Kusini kwa kura ya maoni ya asilimia 63% za wana CCM wa jimbo[5][6]. Akashinda uchaguzi akarudi bunge la Tanzania.[7]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Juni 2017
  2. Profesa Mama Anna Kukohirwa Kajumulo Tibaijuka ni nani? - maisha yake kufuatana na tovuti ya annatibaijuka.org, imeangaliwa Februari 2017
  3. http://www.bbc.com/news/world-africa-30585980
  4. Tibaijuka press conference 18 Dec 2014, report on michuzi blog
  5. Prof Anna K.Tibaijuka ashinda kwa kishindo kura za maoni za chama cha Mapinduzi jimbo la Muleba Kusini Ilihifadhiwa 21 Februari 2017 kwenye Wayback Machine., taarifa kwenye tovuti yake mwenyewe
  6. Tanzania: Kagasheki, Tibaijuka Outshine Opponents in Preferential Elections. report by Tanzania Daily News on 4 August 2015, as per allafrica.com newssite, lookup in February 2017
  7. "Prof Anna Tibaijuka defends her seat as MP of Muleba south constituency in Tanzania Parliament in the 2015 Tanzania Election". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-21. Iliwekwa mnamo 2017-02-23.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: