Angela Merichi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Angela Merichi (21 Machi 1474 – 27 Januari 1540) alikuwa mtawa nchini Italia.
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 27 Januari.
Yaliyomo |
Maisha [hariri]
Angela Merichi alizaliwa eneo liitwalo Desenzano, karibu na mji wa Brescia nchini Italia, tarehe 21 Machi, mwaka 1474.
Alifuata kanuni za Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko, akawakusanya pamoja wasichana, ambao aliwafundisha kutenda matendo ya huruma.
Mwaka 1535, huko Bresha, alianzisha shirika la Waursula, chama cha wanawake waliojishughulisha kuwafundisha wasichana maskini jinsi ya kuwa Wakristo wema.
Alifariki mwaka 1540.
Tazama pia [hariri]
Marejeo [hariri]
- Q. Mazzonis, "The Impact of Renaissance Gender-Related Notions on the Female Experience of the Sacred: The Case of Angela Merici's Ursulines," in Laurence Lux-Sterritt and Carmen Mangion (eds), Gender, Catholicism and Spirituality: Women and the Roman Catholic Church in Britain and Europe, 1200-1900 (Basingstoke, Palgrave Macmillan, 2011),
VIungo vya nje [hariri]
- Catholic Encyclopedia: St. Angela Merici
- Founder Statue at St. Peter's Basilica
- Places in the life of St. Angela Merici
- St. Angela Merici
- Ursuline Sisters of Cincinnati follow her teachings: St. Angela Merici
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Angela Merichi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |