Andy Chande

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jayantilal Keshavji (pia hujulikana kama Andy Chande; 7 Mei 19287 Aprili 2017) alikuwa mfanyabiashara mkubwa, mhisani na mwanachama wa chama cha Freemasons aliyeheshimika kama mtu aliyefanya mambo yenye kuleta matokeo makubwa katika nchi yake ya Tanzania pamoja na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya elimu na ya biashara na masoko.[1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Andy Chande alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shule ya Shaaban Robert Secondary School na rais wa chama cha ‘’Dar es Salaam Secondary Education Society’’. Pia alikuwa mdhamini wa heshima wa shule za jamii ya watu wenye asili ya Uhindi katika mkoa wa Dar es Salaam

Andy Chande amepokea tuzo mbalimbali: mwaka 1998 alipata tuzo kutoka Rotary International ilioitwa ‘’Service Above Self’’ na mwaka 2003 alipokea tuzo ya ‘’Hind Ratna’’ kutoka kwa Waziri Mkuu mstaafu wa India ikiwa ni tuzo ya heshima ya mtu wa mwaka asiyekuwa raia wa India.

Tarehe 10 Agosti 2007, kitabu chake A Knight in Africa” kilichotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili kama Shujaa Katika Afrika: Safari Kutoka Bukene kilizinduliwa na rais wa awamu ya nne nchini Tanzania, Jakaya Kikwete katika ukumbi wa shule ya Shaaban Robert Secondary School, huku marais na watu wengine waliohudhuria siku hiyo akiwemo:

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • Knight Commander of the Most Excellent Order of the British Empire, 2003
  • Pravasi Bharatiya Samman, 2005

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Prominent businessman Andy Chande dies at 88", The Citizen, 2017-04-07. (en) 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Andy Chande kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.