André Brink
André Philippus Brink (amezaliwa tar. 29 Mei 1935 mjini Vrede) ni mwandishi wa riwaya kutoka Afrika Kusini. Anaandika kwa lugha ya Kiafrikana na Kiingereza na ni Profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Cape Town.
Katika miaka ya 1960, yeye na Breyten Breytenbach walikuwa watu muhimu katika harakati ya uandishi ya Kiafrikana iliyoitwa Die Sestigers ("Wa miaka ya sitini "). Waandishi hawa walitazamia kutumia Kiafrikana kama lugha ya kuongea dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi, na pia kufanya fasihi ya Kiafrikana kusukumwa na mienendo ya wakati huo ya fasihi ya Kiingereza na Kifaransa.
Riwaya yake Kennis van die aand ("Maarifa ya Usiku ") (1973) ilikuwa riwaya ya kwanza kupigwa marufuku na serikali ya Afrika Kusini. Brink anaandika vitabu vyake kwa wakati mmoja katika lugha ya Kiingereza na Kiafrikana. Riwaya za mapema za André Brink mara nyingi zilijihusisha na sera za ubaguzi wa rangi. Maandiko yake ya hivi karibuni yanahusu maswala mapya ya kimaisha katika kipindi baada ya ubaguzi nchini Afrika Kusini.
Mwanawe Brink, Anton Brink, ni mchoraji.[1]
Yaliyomo |
Vitabu [hariri]
Kwa orodha kubwa zaidi ya uchapishaji, angalia makala haya ya Kiafrikana André P Brink.
Riwaya [hariri]
- Balozi
- Kutazama Giza
- Wakati katika Upepo
- Fununu za Mvua
- Msimu Mkavu na Mweupe
- Nyororo ya Sauti
- Ukuta wa Ugonjwa Mkubwa
- Hali ya Kidharura
- Teno la Hofu
- Maisha ya Kwana ya Adamastor (1993)
- Kinyume na Hayo
- Kuota kuhusu Mchanga
- Bonde la Shetani
- Haki za Kutamani
- Anderkant die Stilte (2002), ilitafsiriwa kama Upande Mwingine wa Kimya
- Kabla Nisahau (2004)
- Upande Mwingine wa Kimya (2004)
- Panzi (2005)
- Mlango wa Buluu (2006)
- Maisha Mengine (2008)
Vitabu Kuhusu Maisha [hariri]
- Barabara yenye njia mbili (2009)
- Iliripotiwa katika Hope, Christopher (31 Januari 2009). "Traitor to the Tribe". The Guardian. http://www.guardian.co.uk/books/2009/jan/31/fork-in-the-road-review. Retrieved 2 Juni 2009.
Marejeo [hariri]
- ↑ anton brink. South Africian Artists. Rudishwa juu ya 2008-06-27.
- Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
